Makamu wa Rais wa Marekani kufanya ziara Roma na Vatican
18 Aprili 2025Vance atatumia likizo hii ya pasaka kuutembelea mji wa Roma na huko Vatican. Ziara ya Vance nchini Italia inafanyika chini ya kiwingu cha mvutano kati ya Ulaya na Marekani kuhusu hatua ya ushuru iliyochukulikwa na rais Donald Trump pamoja na vita vya Ukraine.
Vance anatarajiwa kukutana na Waziri Mkuu wa Italia Giorgia Meloni, na siku ya Jumapili ya Pasaka, atahudhuria misa katika Kanisa la Mtakatifu Petro. Kuna taarifa kuwa huenda makamu huyo wa rais wa Marekani akakutana na Kiongozi Mkuu wa Kanisa Katoliki Duniani Papa Francis.
Ifahamike kuwa, duru ya pili ya mazungumzo yasiyo ya moja kwa moja kati ya Marekani na Iran kuhusu mpango wa nyuklia wa Tehran inatarajiwa kufanyika huko Roma kesho Jumamosi lakini haijawa wazi ikiwa Vance atashiriki mazungumzo hayo.