Makampuni mawili ya Kimarekani yapewa maagizo ya kuikarabati Iraq:
13 Machi 2004Matangazo
WASHINGTON: Wizara ya Mambo ya Ulinzi ya Marekani imetoa maagizo mawili makubwa mengine ya kibiashara yenye thamani ya Dollar biliyoni moja kwa makampuni ya Kimarekani kuhusu ukarabati wa mfumo wa kusambaza umeme nchini Iraq. Msemaji wa Wizara ya Mambo ya Ulinzi aliarifu mjini Washington maagizo hayo ya kuukarabati mfumo wa umeme wa Iraq imepewa kampuni iitwayo WASHINGTON INTERNATIONAL. Kusini mwa Iraq maagizo hayo itakabidhiwa kampuni ya Kimarekani PERINI. Kila moja ya makampunihayo mawili itapesa maagizo yenye thamanoi ya Dollar miliyoni 500.