You need to enable JavaScript to run this app.
Nenda kwenye maudhui
Nenda kwenye orodha kuu
Nenda tovuti zaidi za DW
Vidio zetu
Sauti zetu
Maeneo
Tanzania
Kenya
Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo
Afrika
Ulaya
Mada
Haki za binadamu
Mazingira
Afya
Teknolojia
Kategoria
Matukio ya Kisiasa
Masuala ya Jamii
Michezo
Yanayoangaziwa
Mzozo wa Kongo Mashariki
Mzozo wa Israel na Hamas
Bundesliga
Sauti zetu
Vidio zetu
Matangazo
Picha: Zoonar/picture alliance
Makala zetu
Sikiliza makala kemkem tulizokuandalia
Ruka sehemu inayofuata Maudhui yote kwenye mada hii
Maudhui yote kwenye mada hii
Matumizi ya lugha ya mkato katika mawasiliano
Vijana mchakamchaka leo inaangazia matumizi ya lugha ya mkato katika maisha ya ya kila siku ya kijana.
Kutana na wanawake mabaharia Tanzania
Makala ya wanawake na maendeleo ya DW inajikita zaidi katika kuwaangalia mabaharia wanawake ambao wameamua kufanya kazi hiyo na kuachana na dhana ya kazi hiyo kuwa ya kiume. Ungana na Anuary Mkama kwa mengi zaidi.
Je, ni salama kujamiiana wakati wa ujauzito?
Zifahamu faida za kiafya za kufanya tendo la ndoa wakati wa kipindi cha ujauzito.
Makala ya Afrika Wiki Hii
Amina Abubakar Mjahid ana mengi katika Makala ya Afrika Wiki Hii, ikiwa ni pamoja na onyo la Rais wa Tanzania Samia Suluhu Hassan kwa watu wanaotaka kuyumbisha usalama wa taifa lake, mashambulizi ya kundi la itikadi kali Mali lasababisha mauaji ya wengi mjini Bamako na pande hasimu sudan zasema ziko tayari kwa mazungumzo ya amani.
Ruto atetea rikodi ya uongozi wake wa miaka miwili
Rais William Ruto wa Kenya ametetea rikodi yake ya miaka miwili madarakani akisema hakuna serikali ya nchi hiyo iliyowahi kuweka mikakati madhubuti ya kuiendeleza Kenya kuliko ile anayoiongoza. Rashid Chilumba alikaa na kiongozi aliekuwa ziarani mjini Berlin, Ujerumani na kujadiliana naye juu ya rekodi hiyo pamoja na mambo mengine.
Familia ya kada wa upinzani aliyeuawa Tanzania yateta
Hivi karibuni nchini Tanzania kumekuwa na matukio ya utekaji watu, kujeruhiwa na wakati mwingine kuuawa. Tukio la hivi karibuni linamhusu kada wa upinzani Ali Kibao aliyekutwa amefariki baada ya kutekwa kabla ya umauti. Sudi Mnette amezungumza na mtoto wake na mjane wake bi Amina Kibao kuhusu kifo cha mumewe katika makala ya Kinagaubaga.
Lishe bora katika kuandaa unyonyeshaji bora
Lishe bora ni kitu cha muhimu wakati mama anapokuwa mjamzito ili kujiandaa kwa ajili ya kumnyonyesha mwanae. Kama wengi tujuavyo, kila mama anahamasishwa kumnyonyesha mtoto wake miezisita ya mwanzo ili kupata lishe bora kabisa anayoihitaji katika ukuaji wake. Kuna mengi ambayo yatakunufaisha ukisikiliza makala ya Afya yako.
Kukatika kwa mawasiliano baina ya marafiki, tatizo ni nini?
Hali ya kupotezeana imekuwa jambo la kawaida hasa baada ya marafiki kuunganishwa kupitia mitandao ya kijamii.
Wanawake na Maendeleo
Bi. Asawar Mustafa, mwanamke mkimbizi kutoka Sudan anayefanya kazi ya ufundi wa magari nchini Libya amefanikiwa kwa vitendo na kuonesha kwamba mwanamke pia anaweza kuwa fundi gereji hodari na kwamba kazi hiyo si ya wanaume pekee. Makala hii imeandaliwa na Zainab Aziz.
Dhulma dhidi ya waandishi habari Kenya
Katika makala ya Mbiu ya Mnyonge leo, mwandishi wa DW Musa Naviye anaangazia dhulma walizopitia waandishi wakati wa maandamano ya kuipinga serikali nchini Kenya. Baadhi ya waandishi walipigwa risasi na kupitia madhila mengine mikononi mwa maafisa wa polisi wakati walipokuwa wakifanya kazi yao ya kuuhabarisha umma.
Sura ya Ujerumani: Umaarufu wa AfD Ujerumani Mashariki
Makala ya Sura ya Ujerumani inamulika je, ushawishi mkubwa wa chama cha AfD mashariki mwa Ujerumani unatokana na nini?
Samwel Daudi na hamasa kwa vijana kukumbatia tamaduni
Kwenye Makala ya Vijana na Uongozi utamsikia kijana anayetaka kuhakikisha vijana wenzake wanabakia kwenye tamaduni za Kitanzania badala ya kubadilishwa na mawimbi ya magharibi. Samwel Daudi anatumia mitandao ya kijamii kuwahamasisha vijana wenzake katika maudhui ya video aliyoyapa jina "Jioni ya Zamani". Sikiliza zaidi kijana huyu akizungumza na Veronica Natalis
Jiunge na Saumu Mwasimba katika Makala ya "Karibuni"
Jiunge na Saumu Mwasimba katika Makala ya "Karibuni"
Umuhimu wa Tembo katika mfumo wa ikolojia
Katika mbuga za wanyama za Tarangire na Manyara mauaji ya tembo yamedhibitiwa. Shirika la Wanyamapori Afrika, AWF linasema hakuna tembo aliyeuawa tangu mwaka 2015 katika maeneo hayo. Lakini unajua faida za tembo kwenye mbuga za wanyama? Ungana na Veronica Natalis kwenye makala haya ya Mtu na Mazingira.
Wanawake na Maendeleo: Jeniffer Shigoli mtetezi wa haki za wanawake na mabinti
Jeniffer Richard Shigoli ni mwanaharakati anaesimamia masuala ya usawa wa kijinsia kupitia kampeni yake ya 'Binti Huru' anawasaidia watoto wa kike walio shuleni waweze kuepukana na vikwazo vitokanavyo na hedhi sabamba na kutoa elimu ya ujasiriamali kwa wanawake walio katika mazingira duni ili waweze kuepukana na umasikini.
Je unasoma masharti wakati wa manunuzi mtandaoni
Sema Uvume je umeshakutana na masharti na makubaliano ama kwa kimobo Terms and Agreements wakati unaponunua vitu mitandaoni? Je, unayasoma na kuyaelewa masharti hayo? Athari za kutoyasoma ni zipi? Sema Uvume inakupa majibu mtayarishaji ni Suleman Mwiru.
Ipi sababu ya kijana kusoma vitabu vya hadithi kuliko dini?
Katika kipindi cha Vijana Mubashara, Jacob Safari anauliza je unafikiri ni kwanini vijana wako radhi kusoma vitabu vya hadithi au riwaya kuliko vitabu vya kidini?
Msimamo wa serikali ya Umoja wa Kitaifa Zanzibar
Ikiwa ni mwaka mmoja kabla ya uchaguzi kufanyika mwakani, mwandishi wetu wa Zanzibar Salma Said, amezungumza na Mwenyekiti wa ACT Wazalendo, ambaye pia ni Makamu wa Kwanza wa Rais wa Zanzibar, Othman Masoud Othman, kujua je juhudi gani ambazo wamezifanya kuinusuru serikali ya umoja wa kitaifa kabla kuporomoka?
Vijana Mchaka Mchaka - Shauku ya kupokea mshahara wa kwanza
Makala ya Vijana Mchaka Mchaka inamulika shauku ya vijana ya kupokea mshahara wa kwanza na umuhimu wa kuuwekea malengo.
Changamoto za uzazi wa mpango nchini Sudan Kusini
Makala ya afya yako inatizama changamoto za upangaji uzazi kwa kundi kubwa la wanawake na wasichana wa Sudan Kusini.
Ukatili wa kingono katika vita vya Sudan
Mbiu ya Mnyonge hivi leo inalia na wanawake wa Sudan wanaoandamwa na ukatili wa kingono katikati mwa balaa la vita.
09.08.2024 Kipindi cha "Karibuni" na Jay Masai
Katika kipindi cha "Karibuni" cha 09.08.2024 utamsikia Jay Masai, mwanamuziki wa miondoko ya Hip hop wa Kenya.
Maandamano ya vurugu Uingereza
Uingereza inakabiliwa na maandamano ya vurugu kufuatia mauaji ya wasichana watatu mnamo Julai 29 huko Southport. Washiwishi wa mitandaoni wenye mafungamano na itikadi za siasa kali za mrengo wa kulia walizagaza uvumi kuhusu mhusika wa mauaji hayo na kusema ni muislamu mwenye itikadi kali aliyewasili Uingereza hivi karibuni, na hivyo kuchochea chuki dhidi ya wahamiaji na waislamu nchini humo.
Mpenzi aliyetengenezwa kwa teknolojia ya Akili Mnemba
Kama ungepata nafasi ya kumtengeneza mwenyewe mwenzi wako kwa namna unayotaka mwenyewe, ungependa awe vipi? Teknolojia ya Akili Mnemba sasa inatumiwa kutengeneza mpenzi mwenye sifa na hulka anayoitaka mtu. Fuatilia hapa katika makala ya Sema Uvume.
Tuzo za fasihi na waandishi wanawake wa Kiafrika
Tuzo ya Fasihi ya Safal-Cornell inakaribia kutimiza miaka 10 tangu ilipoasisiwa mwaka 2014 na washindi wake wa kwanza kutangazwa mwaka 2015. Tuzo hiyo imevutia ushiriki wa maelfu ya wanafasihi kwenye mataifa yanayozungumza Kiswahili. Mohammed Khelef anazungumza na Anna Samuel, mshindi wa kwanza aliyeizindua tuzo hiyo ya riwaya yake ya Penzi la Damu, juu ya safari ya mwandishi wa fasihi.
Sudan: Je makubaliano ya kuvimaliza vita yanaweza kufikiwa?
Zainab Aziz amewakaribisha wachambuzi kuijadili hali ya Sudan ambako majenerali wawili wanapigana kuidhibiti nchi hiyo.
Fahamu kuhusu wizi wa taarifa binafsi mtandaoni
Wizi wa taarifa binafsi ni uhalifu wa mtandaoni ulioshamiri nyakati hizi dunia ikishuhudia maendeleo makubwa ya teknolojia. Sambamba na tatizo hilo, makala ya Sema uvume leo inaangazia pia wimbi kubwa la ujumbe mfupi unaolenga kuwahadaa na kuwaibia watu. Sikiliza hapa kufahamu zaidi
Belarus: Miaka 30 ya utawala wa Lukashenko
Katika siasa za ulaya kwa miongo kadhaa, tumeshuhudia viongozi wa mataifa mbalimbali wakipishana madarakani. Lakini Alexander Lukashenko amekuwa rais wa Belarus kwa miaka 30. Kiongozi huyo mwenye umri wa miaka 69, ameitawala nchi hiyo kwa mkono wa chuma na kuwa na udhibiti kamili. Kipi kimemuwezesha kusalia madarakani kwa muda wote huo? Ni mbinu gani anazozitumia ili kutoyumbishwa?
Habineza: Nilijitabiria kupata angalau asilimia 55 ya kura
Aliyekuwa mgombea wa uchaguzi wa rais uliomalizika nchini Rwanda Frank Habineza aliyeibuka nafasi ya pili kwa kupata asilimia 0.5 amezungumza na Rashid Chilumba katika Kinagaubaga. Ameeleza kuwa alikuwa na matarajio ya kupata asilimia nyingi katika uchaguzi huo.
Kinagaubaga: Tume ya uchaguzi nchini Tanzania ni huru?
George Njogopa anazungumza na Mkurugenzi wa Tume ya Uchaguzi nchini Tanzania, Ramadhan Kailima kuhusu uboreshaji daftari la wapigakura, malalamiko ya upinzani kutoshirikishwa kwenye michakato ya tume na ikiwa ni kweli tume hiyo ya kusimamia uchaguzi ni huru.
Jukwaa la Manufaa
Angela Mdungu anakupa nafasi ya kutoa dukuduku pongezi, maoni au ushauri kuhusu masuala yanayohusu jamii inayokuzunguka.
Wakenya wageukia dawa za kiasili na kuacha za hospitalini
Wimbi la madadiliko linazidi kupepea nchini Kenya, na kila linapopita linaleta athari chanya, likibadilisha mawazo ya wakenya wengi wanaokumbatia dawa za kiasili na kuachana na dawa za hospitalini. Shisia Wasilwa anakufahamisha ni kwanini hilo linashuhudiwa nchini humo.
Uhaba wa wafanyakazi wenye ujuzi Ujerumani
Uhaba wa wafanyakazi wenye ujuzi Ujerumani unavyokwamisha shughuli mjini Mittweida
Mitandao ya kijamii inaweza kuleta mageuzi ya siasa Afrika?
Makala ya Vijana Mchaka Mchaka inamulika nafasi mitandao ya kijamii barani Afrika katika mageuzi ya kisiasa.
Msigwa: Chadema imepoteza mwelekeo wake wa kisera
Kambi ya upinzani nchini Tanzania imepata pigo kubwa baada ya mwasiasa mkongwe wa upanzani mMchungaji Peter Msigwa kutimkia chama tawala CCM huku akitangaza chama chake cha zamani kukosa mwelekeo katika masuala kadhaa ikiwemo demokrasia na mwelekeo wa kisera, lakini anakoselewa kuwa ni mwanasiasa mwenye uchu wa madaraka. Msikilize akijibu tuhuma hizi
Vikosi vya Tanzania vitaendelea kubaki Msumbiji
Katika wasaa huu wa takriban dakika kumi Sudi Mnete anazungumza na waziri wa Ulinzi nchini Tanzania Stergomena Tax kutaka kujua mwenendo wa oparesheni ya kijeshi ya vikosi vya Tanzania nchini Msumbiji.
Waasi wa M23 wakanusha kushirikiana na jeshi la Rwanda
Jeshi la Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo na waasi wa M23 wameweka chini mtutu wa bunduki ili kupisha misaada ya kiutu kuingia katika maeneo yanayoshuhudia mapigano makali. Hatua hii inafanyika katika wakati ambapo Rwanda inashutumiwa kupeleka vikosi vyake kupigana mashariki mwa Kongo, je Kigali inaunga mkonoM23?. Katika Kinagaubaga sikilize msemaji wa M23
Umasikini unavyowatesa wastaafu Germany
Mstaafu mmoja kati ya watano nchini Ujerumani anakabiliwa kuwa katika hatari ya umasikini, kulingana na ofisi ya takwimu ya Ujerumani. Idadi ni kubwa zaidi hasa kwa upande wa wanawake
Akili mnemba katika soka
Makala ya Sema Uvume leo inamulika namna akili mnemba inavyotumika na inavyotarajiwa kutumika katika maeneo mbalimbali ya mpira wa miguu.
Mabadiliko ya uongozi kwenye Jumuiya ya kijeshi ya NATO
Kwa mujibu wa taarifa, Waziri Mkuu wa Uholanzi Mark Rutte, anatarajiwa kuwa Katibu Mkuu mpya wa jumuiya ya kujihami ya NATO baada ya mpinzani wake rais wa Romania Klaus lohannis, kujoindoa kwenye kinyangànyiro. Mtayarishaji Zainab Aziz
Kujikolonisha kwa wasomi wa Kiafrika
Mohammed Khelef anazungumza na Profesa Mutembei juu ya dhana ya "kujikolonisha" miongoni mwa wasomi wa Kiafrika.
Raia wa Sudan wakabiliwa na madhila ya vita
Raia wa Sudan wanakabiliwa na usalama mdogo, ukosefu wa chakula, maji safi na huduma nyingine muhimu.
22.06.2024: Taarifa ya Habari ya Asubuhi
Ungana nasi asubuhi hii ksikiliza Taarifa ya Habari. Miongoni mwa nyinginezo utasikia kuhusu ziara ya Waziri wa uchumi wa Ujerumani huko nchini China katikati ya mvutano kuhusiana na ushuru wa magari yanayotumia umeme, Uholanzi kuipatia Ukraine mfumo wa kujilinda angani na Korea Kusini yamwita balozi wa Urusi huku mvutano ukiongezeka na Korea Kaskazini.
Mtu mmoja auwawa katika maandamano ya nchini Kenya
Kenya yatikiswa na maandamano makubwa katika mji mkuu Nairobi na miji mingine ya kupinga muswaada wa fedha. Mahujaji 658 wa Misri ni miongoni mwa waumini waliopoteza maisha kufuatia joto kali huko Makkah. Wabunge nchini Kongo wakubali kupunguziwa mishahara yao ya dola elfu 21 hadi dola elfu 5 katika tukio la aina yake. Jiunge na Saumu Mwasimba katika Afrika wiki hii hapa DW kiswahili.
Masuluhisho kupitia habari
Mjadala juu ya nafasi ya vyombo vya habari vya Afrika kusaka masuluhisho ya matatizo ya Kiafrika.
Ajenda ya Tanzania ya kufanikisha nishati safi ya kupika kwa wote barani Afrika
Ajenda ya nishati safi kwa wote ya Tanzania ilivyogeuka kuwa ya kimataifa katika mkutano wa mazingira wa Bonn.
Ipi hatima ya Ulaya baada ya uchaguzi wa bunge la Ulaya?
Katika Maoni mbele ya Meza ya Duara, Mohammed Khelef amewashirikisha wadau kadhaa kuzungumzia mafanikio yaliyopatikana kwa vyama vya siasa kali za mrengo wa kulia katika uchaguzi wa bunge la Ulaya.
Matokeo ya Uchaguzi wa Bunge la Ulaya
Uchaguzi wa Bunge la Ulaya ulifanyika kuanzia tarehe 6 hadi 9 Juni 2024 katika jumla ya mataifa 27 ya Umoja huo. Matokeo ya uchaguzi huo yalikuwa pigo kubwa kwa vyama vya jadi, kutokana na vyama vya siasa kali za mrengo wa kulia na vile vya kizalendo kupata matokeo mazuri. Hata hivyo vyama vya kihafidhina vilishinda uchaguzi huo. Ungana na Bakari Ubena katika kipindi hiki cha Mwangaza wa Ulaya.
Germany inakabiliana vipi na uhalifu wa ukoloni Tanzania?
Ujerumani bado inaendeleza juhudi zake za kujivua gamba na yaliyotokea katika kipindi cha ukoloni nchini Tanganyika ambayo ni Tanzania bara ya sasa, mafuvu kadhaa ya binadamu walionyongwa yalisafirishwa kutoka nchini humo hadi Ujerumni kuhifadhiwa. Sasa familia za wahusika wameweka madai mezani. Sikiliza mahojiano.
Unafahamu kumudu kuongea lugha zaidi ya tatu ni mtaji?
Wataalamu mbalimbali wanasema watu wengi duniani wanaweza kumudu kuzungumza walau lugha zaidi ya mbili kwenye maisha yao duniani. kufahamu lugha kunatajwa kuwa ni nyenzo muhimu kwako kijana kufungua fursa. Je unaongea lugha ngapi?
Ukurasa uliotangulia
Ukurasa 4 wa 6
Ukurasa unaofuatia