You need to enable JavaScript to run this app.
Nenda kwenye maudhui
Nenda kwenye orodha kuu
Nenda tovuti zaidi za DW
Vidio zetu
Sauti zetu
Maeneo
Tanzania
Kenya
Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo
Afrika
Ulaya
Mada
Haki za binadamu
Mazingira
Afya
Teknolojia
Kategoria
Matukio ya Kisiasa
Masuala ya Jamii
Michezo
Yanayoangaziwa
Mzozo wa Kongo Mashariki
Mzozo wa Israel na Hamas
Bundesliga
Sauti zetu
Vidio zetu
Matangazo
Picha: Zoonar/picture alliance
Makala zetu
Sikiliza makala kemkem tulizokuandalia
Ruka sehemu inayofuata Maudhui yote kwenye mada hii
Maudhui yote kwenye mada hii
DeepSeek Akili Mnemba iliyoteka soko la teknolojia
DeepSeek imeleta mapinduzi katika mukhtadha wa teknolojia ya Akili Mnemba kutokana na namna ambavyo inachakata taarifa zake, lakini upo wasiwasi wa namna inachakata data zake, wataalamu wanaonya kuwa inaweza kutumiwa vibaya katika kutoa taarifa.
Matetemeko ya ardhi yasababisha hofu nchini Ugiriki
Tangu mwanzoni mwa mwezi Februari kumeshuhudiwa mkururo wa matetemeko ya ardhi nchini Ugiriki hasa katika kiswa cha Santorini na kuzusha hofu kulipuka kwa volkano katika siku za usoni. Makala ya Mwanza wa Ulaya inatuama hapo nahodha ni Bakari Ubena
Makala ya Afrika Wiki Hii
Mzozo wa Mashariki mwa Kongo unaendelea kufukuta na viongozi wa M23 walijitokeza hadharani kuzungumza na wakazi wa Goma. Mataifa ya Afrika yajiandaa kukabiliana na uamuzi wa Rais wa Marekani Donald Trump wa kusitisha misaada kwenye mashirika ya kigeni. Tutaumulika mzozo wa Sudan, mripuko wa ugonjwa hatari wa Ebola nchini Uganda na mengine mengi.
Ijue saratani ya shingo ya kizazi na madhara yake
Ripoti za utafiti wa kisayansi zimeafiki kuwa saratani za shingo ya kizazi hutokana na maambukizi ya virusi vya 'Human Papillomavirus' au HPV vilivyoko katika jamii ya papilloma. Kwa mujibu wa WHO ulimwenguni kote saratani ya shingo ya kizazi ni saratani ya nne kwa kuathiri wanawake.
Vikundi vya kuweka fedha kwa ajili ya safari za kitalii
Vijana wanaunga makundi kwa ajili ya kutunza fedha kwa pamoja ili kufanikisha safari zao za kitalii, katika mtindo huu unaoanza kuvuma kwa kasi kwa mataifa ya Afrika, vijana wengi wamefanikisha malengo yao ya kutalii maeneo mbalimbali ulimwenguni
Meza ya Duara: CHADEMA mikononi mwa Lissu
CHADEMA inasema kwamba bila mabadiliko kwenye sheria za uchaguzi hakutakuwa na uchaguzi wa Oktoba 2025.
Maoni: Kuna nini Congo?
Rais wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo Félix Tshisekedi amewatolea wito vijana wajitokeze kwa wingi wajisajili jeshini kusaidia kupambana na waasi wa kundi la M23 wanaoudhibiti mji wa Goma. Kuna nini Congo? Je, vita kamili vimeanza? Congo yaelekea wapi? Sikiliza kipindi cha Maoni kikiongozwa na Josephat Charo.
Je, Rais Biden atakumbukwa kwa yapi?
Kuanzia kuimarisha mahusiano kati ya Marekani na Afrika, usuluhishi wa mgogoro wa Sudan, mageuzi katika taasisi za kimataifa, vita vya Mashariki ya Kati na Ukraine hadi juhudi za kudhibiti ugonjwa wa corona - Joe Biden atakumbukwa kwa mengi - mafanikio aliyoyapata na alivyokwama kuwa rais wa Marekani kwa awamu ya pili. Jiunge na Josephat Charo katika kipindi cha Maoni.
Kinyang'anyiro cha makamu mwenyekiti ndani ya Chadema
Nchini Tanzania, joto la kisiasa ndani ya chama cha demokrasia na maendeleo Chadema linazidi kushika kasi kabla ya CHADEMA kupata safu yao mpya ya Uongozi wa Juu. Vuta nikuvute ipo pia kwenye nafasi ya makamu mwenyekiti. Kwenye kinagaubaga, Dotto Bulendu anazungumza na Ezekiel Wenje, mmoja wa wagombea wa nafasi hiyo. Sikiliza
Mwangaza wa Ulaya: Jukumu la FPÖ kuunda serikali Austria
Chama cha siasa kali za mrengo wa kulia nchini Austria cha FPÖ kinachoongozwa na Herbert Kickl kimepewa kwa mara ya kwanza katika historia, jukumu la kuongoza mazungumzo ya kuunda serikali baada ya vyama vya jadi kushindwa kuafikiana. Katika hali ya kushangaza, chama cha kihafidhina cha OVP kimekubali kujiunga na FPÖ kwenye mazungumzo hayo.
Maoni Mbele ya Meza Duara: Matukio ya Utekaji Kenya na Tanzania
Kumekuwepo na matukio yanayodaiwa kuwa ni ya utekaji nyara watu katika maeneo ya nchi za Afrika Mashariki za Kenya na Tanzania. Matukio hayo yamesababisha hofu. Watalaamu wamelijadili swala hilo. Mtayarishaji Zainab Aziz
Othman Masoud Othman atangaza nia ya kuwania urais Zanzibar
Makamu wa Kwanza wa Rais wa Zanzibar Othman Masoud Othman atangaza nia ya kuwania urais kwa mara ya kwanza.
Afrika katika magazeti ya Ujerumani
Yaliyozingatiwa na magazeti ya Ujerumani mnamo wiki hii ni pamoja na maandamano ya vijana yamepamba moto nchini Msumbiji kudai mabadiliko ya uongozi. Juu ya ugonjwa usiojulikana nchini Jamuhuri ya Kidemokrasia ya Kongo. Kuangushwa kwa Assad kunaweza kutatiza shughuli za Urusi nchini Libya na kwenye ukanda wa Sahel. Mtayarishaji, Zainab Aziz
Shule ya Msitu wa Tembo yasaidiwa taa za nishati ya jua
Wanafunzi wafunga taa za nishati ya jua katika shule ya Msitu wa iliyopo Simanjiro Manyara kaskazini mwa Tanzania.
Mwangaza wa Ulaya: Mapitio ya mwaka 2024
Katika kipindi hiki maalum ambapo tutasafiri wote kwa muda wa dakika ishirini kuyakumbuka mambo muhimu yaliyotokea barani Ulaya mnamo mwaka huu wa 2024 uliogubikwa na masuala ya siasa, mabadiliko ya uongozi katika taasisi muhimu, vita vinavyiendelea nchini Ukraine, chaguzi mbalimbali, mafuriko, mioto ya nyika, na hata michezo. Ungana na Bakari Ubena.
21.12.2024: Matangazo ya Asubuhi
Ungana nasi hapa kusikiliza yaliyomo asubuhi hii kwenye uchambuzi na makala nzuri kabisa tulizokuandalia ikiwa ni pamoja na makala ya Afrika Wiki Hii, ujue yaliyoandikwa zaidi na kupewa kipaumbele kote barani Afrika kwa wiki hii nzima.
Jukwaa la Manufaa
Sikiliza maoni yako msikilizaji katika kipindi cha Jukwaa la Manufaa, kilichoandaliwa na kuongozwa na Selina Mdemu.
Matangazo ya Mchana 15.12.2024
Miongoni mwa mengineyo utakayoyasikia kwenye matangazo ya mchana ni pamoja na Marekani imesema imefanya mawasiliano ya moja kwa moja na utawala mpya wa Syria: Rais wa mpito nchini Korea Kusini awaahidi washirika wake kuimarisha upya masoko ya fedha na Ukraine yasema wanajeshi wengi zaidi wa Korea Kaskazini wanapambana Kursk. Utasikia pia makala mbalimbali ikiwa ni pamoja na Afrika Wiki Hii.
Harakati za mjasiriamali Jackline Machoke
Makala ya wanawake na maendeleo mara hii inamuangazia mjasiriamali Jackline machoke kutoka Tanzania na namna anavyoitumia nafasi yake kuwainua wajasiriamali wengine na kuwasaidia wasiojiweza. Ambatana naye Angela Mdungu kufahamu zaidi.
Kinagauba: Machafuko ya kisiasa Msumbiji baada ya uchaguzi
Sudi Mnette amezungumza na Manuel Gabriel Aidao Miandica kuhusu hali ya machafuko ya baada ya uchaguzi nchini Msumbiji.
Maoni: Uchaguzi wa serikali za mitaa Tanzania ulikuwa huru?
Kipindi cha Maoni wiki hii kinajadili iwapo uchaguzi wa serikali za mitaa nchini Tanzania ulikuwa huru na wa haki.
Unyanyapaa dhidi ya watoto wanaozaliwa na vichwa vikubwa
Makala ya mbiu ya mnyonge inauangazia kwa kina unyanyapaa unaowakumba wazazi pamoja na watoto wanaozaliwa na ulemavu wa kichwa kikubwa na na mgongo wazi. Wengi wanadai kutengwa na baadhi ya watu. Anwary Mkama amezungumza na baadhi ya familia zinazowalea watoto hao.
Teknolojia inayowasaidia watoto kusoma na kuandika
Wadau katika sekta ya elimu nchini Kenya wameanzisha kampeni inayolenga kutumia teknolojia na mbinu za kidigitali kuhimiza utamaduni wa kusoma miongoni mwa watoto ili kuboresha elimu ya utotoni na viwango vya kuandika. Wakio mbogho ana anasimulia zaidi katika makala hii ya Sema Uvume.
Nondo anaeleza Kinagaubaga baada ya kutekwa na Wasiojulikana
Katika mahojiano ya Kinagaubaga Rashid Chilumba anazungumza na Mwenyekiti wa Ngome ya Vijana wa chama cha upinzani Tanzania ACT-Wazalendo, Abdul Nondo ambane anaelezea kwa kina kutekwa kujeruhiwa na kisha kutupwa katika ufukwe wa Bahari ya Hindi, jijini Dar es Salaam.
Nini maana ya 'tabia bwete'?
Tabia bwete ni hali ya kushinda ukilaza damu bila ya kujishughulisha na mambo yanayoweza kukuletea kipato. Je vijana nchini Tanzania wanazungumziaje tabia hiyo? Wasukilize vijana wa Dar es Salaam kwenye kipindi cha Vijana Tugutuke.
Kinagaubaga na Naibu Waziri Mkuu wa Tanzania Dotto Biteko
Naibu Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dotto Biteko amesema maaandalizi ya uchaguzi wa serikali za mitaa kwa Novemba 2024 yalifanyika kwa muda mrefu na uchaguzi huo umekua na hamasa kubwa.
Duru ya kwanza ya uchaguzi wa rais Romania
Duru ya kwanza ya uchaguzi wa rais nchini Romania ilifanyika Jumapili ya Novemba 24 na matokeo yake yaliushangaza ulimwengu baada ya ushindi wa mgombea ambaye hakutegemewa kabisa. Mgombea huru Calin Georgescu mwenye umri wa miaka 62 anayetajwa kuwa na siasa kali za mrengo wa kulia aliibuka mshindi kwa kujipatia asilimia 22.94 ya kura, huku nafasi ya pili ikishikiliwa na Elena Lasconi.
Katika mahojiano ya Kinagaubaga Meya wa Jiji la Dar es S
Katika mahojiano ya Kinagaubaga Meya wa Jiji la Dar es Salaam Omar Kumbilamoto amezungumza na DW kuhusu hali ya majengo
Ni kwanini vijana wameyapa kisogo mapishi?
Kwa taratibu za Kiafrika, shughuli mojawapo ya nyumbani anayopaswa kuijua na kuifanya kijana ni kupika. Lakini kwa sasa vijana hasa wa maeneo ya miji mikubwa hawafahamu kupika. Sikiliza makala ya vijana mchakamchaka kufahamu zaidi kuhusu mada hii.
Mfumo wa kidijitali wa matumizi ya maji
Maji Smarti ni mfumo wa kielektroniki unaowezesha kutoa taarifa za kiwango cha maji kilichopo katika chanzo husika, pamoja na kugundua kama kuna uharibifu wa miundombinu ya maji. Mfumo huu umetengenezwa na wanafunzi wa kidato cha sita kutoka Shule ya Sekondari ya Arusha Sayansi, iliyoko kaskazini mwa Tanzania, na tayari umeanza kutumika shuleni hapo.
Unalijua tatizo la Shoulder impingement Syndrome?
shoulder Impingement Syndrome inatokea pale mifupa katika bega lako inaposuguana au kubana katika misuli, na kufanya sehemu hiyo kuwa na maumivu makali. Makala ya Afya Yako inaliangazia zaidi tatizo hilo pamoja na tiba yake.
Makala ya Afrika Wiki Hii
Amina Abubakar ana mengi katika Makala ya Afrika Wiki hii, ikiwemo kile kinachoendelea Marekani, Donald J Trump kurejea tena madarani kama rais wa 47 wa taifa hilo. Je ushindi wake una maana gani kwa Bara la Afrika? Nchini Msumbiji ghasia za baada ya uchaguzi zashuhudiwa na Kongo na Rwanda zathibitisha haja ya kuheshimu usitishaji mapigano mashariki mwa Kongo.
"Kusaidia hakuhitaji uwe tajiri au kupato kikubwa"
Je ni kwa umbali gani unaweza kuwasaidia watu wasiokuwa na uwezo kiuchumi katika jamii yako ikiwa mwenyewe huna ajira? Cecilia kijana wa miaka 27 asiyekuwa na ajira anahangaika kuisadia jamii yake ya Turkana akitembea nyumba hadi nyumba kutowa msaada wa kile kidogo anachopata.Ndani ya karibuni utamsikia akisimulia kipi kilichomsukuma kuanza jitihada hizo.
Utamaduni na Sanaa: Waturkana na tamasha la Tobongulore
Neno "Tobongulore" lina maana ya karibu nyumbani, kwani inasadikika kuwa eneo la Turkana ndilo chimbuko la binadamu.
Vifaa duni vyaathiri huduma kwa wenye magonjwa ya damu
Jukwaa la Viongozi wa magonjwa ya damu limefanyika huku miundombinu duni ya afya, ukosekanaji wa wataalamu wa afya na upungufu wa vifaa tiba vikitajwa kuwa ndicho chanzo cha matibabu na usimamizi duni kwa wenye magonjwa ya damu, Afrika Mashariki. Mwenzetu Florence Majani alihudhuria jukwaa hilo na kutuandalia taarifa hii.
26.10.2024: Matangazo ya Asubuhi
Ungana nasi hapa kusikiliza Matangazo ya Asubuhi kuanzia uchambuzi wa ripoti zetu kwa kina hadi makala ambazo ni pamoja na Afrika Wiki Hii na Vijana Tugutuke. Tafadhali sikiliza hapa.
25.10.2024: Taarifa ya Habari ya Asubuhi
Miongoni mwa yaliyomo kwenye taarifa ya habari ya asubuhi ni Rais wa urusi Vladimir Putin ahitimisha mkutano wa kilele wa kundi la BRICS: Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Antonio Guterres asema uvamizi wa Urusi nchini Ukraine ni kinyume cha sheria: Na Bahamas yataka mazungumzo ya kweli kuhusu fidia kutokana na historia ya utumwa. Ungana nasi.
Kinagaubaga kwa ripoti ya HRW na majibu ya Profesa Kabudi
Kinagaubaga kuhusu ripoti ya Human Rights Watch kwa Tanzania na majibu ya Waziri wa Katiba na Sheria Palamagamba Kabudi.
24.10.2024: Taarifa ya Habari ya Asubuhi
Miongoni mwa habari tulizonazo asubuhi hii ni Ujerumani na Austria zawaita mabalozi wa Korea Kaskazini kufuatia tuhuma za kuwapeleka wanajeshi wake nchini Urusi. Ufaransa yanuia kukusanya dola milioni 540 kwa ajili ya kuisaidia Lebanon na Watu watano wauawa na wengine 22 kujeruhiwa katika shambulizi kwenye kiwanda cha vifaa vya ndege nchini Uturuki. Ungana nasi.
Mapambano dhidi ya ufisadi Kenya
EACC Kenya inawachunguza maafisa 67 wa ngazi za juu katika kaunti, ikiwa ni sehemu ya kesi 231 za ufisadi zinazoendelea
Mwalimu Nyerere, kiongozi adimu mwenye maono
Mnamo wiki hii Watanzania wamemkumbuka kiongozi wao adhimu, Mwalimu Julius Nyerere aliyeaga dunia miaka 25 iliyopita baada ya kuwaachia watanzania na waafrika kwa jumla turathi za milele: uhuru wa Tanganyika, Muungano wa Tanzania, Umoja wa nchi za Afrika,OAU na ukombozi wa kusini mwa Afrika. Wataalamu wetu wameyajadili hayo na mengine mengi kwenye meza ya duara.
Mradi wa Shanga Shanga
Ushawahi kufika eneo la Shanga Shanga? Ni eneo maarufu Arusha, Tanzania ambako bidhaa za shanga, bilauri za vioo, pamoja na nguo zinakotengenezwa. Karibu 80% ya wafanyakazi katika eneo hili ni watu wenye ulemavu. Umaarufu wake zaidi ni kutokana na kuwa malighafi ya bidhaa zinazotengenezwa hapa ni rafiki kwa mazingira. Takataka ndiyo malighafi kuu. Msikilize Anuary Mkama katika Mtu na Mazingira.
Uwezo wa dawa za kiasili na usalama wake Kenya
Wagonjwa zaidi wanaougua magonjwa sugu wanaripoti hali yao ya kiafya kuimarika baada ya kugeukia dawa za kiasili. Wadau kwenye sekta hii wanasema kuna haja ya kuwianisha dawa za kiasili na za kisayansi ili kuupiga jeki mfumo wa afya nchini Kenya. Makala ya afya yako hii inajikita kwenye mada hii na mwandishi na msimulizi ni Wakio Mbogho.
Ukiukaji wa haki za binadamu Kenya
Serikali ya Rais aliyeko madarakani Kenya William Ruto inakosolewa kwa ukiukaji mkubwa wa haki za binadamu miaka miwili tangu ilipoingia madarakani. Zaidi ya mauaji 128 ya kiholela yamerekodiwa na visa 351 vya unyanyasaji kuripotiwa na mashirika ya kutetea haki za binadamu tangu mwaka 2022. Wakio Mbogho anajikita kwenye suala hili katika makala hii ya Mbiu ya Mnyonge.
Saidi Nguba "Edward Moringe Sokoine: Maisha na Uongozi wake"
Hivi karibuni kumefanyika uzinduzi wa kitabu cha Waziri Mkuu wa zamani wa Tanzania, Hayati Edward Moringe Sokoine: Maisha na Uongozi wake.Kitabu hicho kimezungumzia maisha ya kiongozi huyo na urathi wa kisiasa na kiuongozi aliowaachia Watanzania. Kitabu hicho kilichoandikwa na waandishi nguli wa habari Salva Rweyemamu na Saidi Nguba. Rashid Chilumba alipata fursa ya kuzungumza na Nguba, msikilize.
Mabadiliko katika tamasha la Oktobafest nchini Ujerumani
Sura ya Ujerumani wiki hii inaangazia Halfa ya kila mwaka, maarufu kwa jina la tamasha la oktoba, (Oktoberfest) katika jimbo la Bavaria, kusini mwa Ujerumani, lililomalizika mwishoni mwa wiki iliyopita.
Vijana na Uongozi: Noel, mmiliki wa kampuni ya maparachichi
Noel Lugenge anamiliki na kusimamia kampuni yake mwenyewe ya kilimo na usafirishaji wa maparachichi nchini Tanzania.
Makala: Wakimbizi wa ndani wageukia kilimo Kongo
Benjamin Kasembe anaangalia jinsi wakimbizi waliopo mjini Goma wanavyoendeleza kilimo kama njia ya kujikimu kimaisha.
Mazingira: Ziwa Turkana lafurika
Michael Kwena anasimulia majaliwa ya ziwa hilo muhimu kwa Wakenya.
Fahamu namna ya kujenga uelewa kuhusu kuzuwia kujitoa Uhai
Kulingana na takwimu za shirika la afya ulimwenguni WHO, zaidi ya watu laki saba hukatisha uhai wao kila mwaka kwa kudhamiria. Je ni nini hasa kinamfanya mtu kujitoa uhai, Makala ya Afya yako inafafanua hilo. Mtayarishaji ni Amina Abubakar.
Ukurasa uliotangulia
Ukurasa 3 wa 6
Ukurasa unaofuatia