You need to enable JavaScript to run this app.
Nenda kwenye maudhui
Nenda kwenye orodha kuu
Nenda tovuti zaidi za DW
Vidio zetu
Sauti zetu
Maeneo
Tanzania
Kenya
Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo
Afrika
Ulaya
Mada
Haki za binadamu
Mazingira
Afya
Teknolojia
Kategoria
Matukio ya Kisiasa
Masuala ya Jamii
Michezo
Yanayoangaziwa
Mzozo wa Kongo Mashariki
Mzozo wa Israel na Hamas
Bundesliga
Sauti zetu
Vidio zetu
Matangazo
Picha: Zoonar/picture alliance
Makala zetu
Sikiliza makala kemkem tulizokuandalia
Ruka sehemu inayofuata Maudhui yote kwenye mada hii
Maudhui yote kwenye mada hii
Chama kipya cha Gachagua kitashawishi vipi siasa za Kenya?
Aliyekuwa, naibu wa rais wa Kenya, ambaye hivi sasa ni kiongozi mkuu wa chama cha Democracy for Citizens Party (DCP), Rigathi Gachagua, ameendelea kuimarisha safari zake za kampeni kukinadi chama chake kipya. Je, chama hiki kipya kitakuwa kikubwa kiasi gani kuweza kuwa na ushawishi katika siasa za Kenya kuelekea uchaguzi mkuu ujao? Jiunge na Josephat Charo katika kipindi cha Maombi mbele ya Duara.
Unathibitisha vipi taarifa ndani na nje ya mitandao?
Ni kwa namna gani mtumiaji wa mtandao wa kijamii anaweza kujilinda na taarifa za uwongo? Sema uvume inakupa jibu kwa kuliangazia Jukwaa la mtandaoni la Jamii check, linalotumika kusaidia kutambua ukweli wa taarifa zinazopatikana mitandaoni.
Maoni: Kabila arejea nchini Kongo hatua hiyo ina maana gani
Rais wa zamani wa nchini Jamuhuri ya Kidemokrasia ya Kongo, Joseph Kabila, anayetuhumiwa kuwaunga mkono waasi wa M23 wanaodhibiti eneo la Mashariki mwa Kongo amerejea nchini humo na kwenda kwenye eneo hilo. Je! maana yake ni nini? na hasa baada ya bunge kumvua Kabila, hadhi ya kisheria ya kumkinga dhidi ya mashtaka. Mwenyekiti ni Zainab Aziz
Makala ya Afrika wiki hii
Wanaharakati wa Kenya na Uganda, Boniface Mwangi na Agatha Atuahire waachiwa huru wakiwa hali dhaifu baada ya kushikiliwa siku kadhaa na maafisa wa usalama wa Tanzania. Rais wa zamani wa DRC Joseph Kabila aondolewa kinga ya kushtakiwa huku akituhumiwa kwa uhaini na serikali. Na ziara ya rais Cyria Ramaphosa Afrika Kusini pia ni sehemu ya yaliyoangaziwa barani Afrika wiki hii.
Wazazi na kudhibiti matumizi ya mitandao kwa watoto
Watoto wanakuzwa katika mazingira yaliyojaa teknolojia ambayo imekuwa sehemu ya maisha yao. Kando na teknolojia kuwa na faida pia ina athari chungu nzima. Swali ni je, wazazi wana uelewa wa kutosha wa kusimamia matumizi sahihi ya teknolojia kwa njia salama?
Reichsbürger: Vuguvugu lililo na msimamo mkali Ujerumani
Vuguvugu la Reichsbürger la nchini Ujerumani, ni muungano wa makundi kadhaa na watu binafsi yenye msimamo mkali yasiyoitambua serikali ya Ujerumani. Vuguvugu hili linalodai utawala wa Kifalme, lilianzishwa rasmi mwaka 1980.
Ipi tofauti ya sonona, msongo wa mawazo na afya ya akili?
Afya ya akili ni hali ya jumla ya ustawi wa akili kihisia, na inahusiana na uwezo wa mtu katika kufikiri, kuhisi na kudhibiti hisia. Hakuna tofauti kubwa sana kati yake msongo wa mawazo na Sonona. Makala ya Afya yako ina mengi zaidi.
Tangalizi - chakula cha Waswahili wa pwani
Ladha ya kumbukumbu, harufu ya utamaduni, na mvuto wa mila zetu... Je, umewahi kusikia kuhusu chakula cha siri kinachopikwa kwa hafla maalum tu? Jua hadithi yake na kwanini kizazi kipya kina hofu kwamba inaweza kusahaulika kabisa.
Mlipuko wa Kalazar Kenya - Je, Afrika inashidwa wapi?
Kenya inakabiliwa na mlipuko hatari wa ugonjwa wa Kalazar, ambapo watu 33 wamefariki na zaidi ya visa 1,000 vimeripotiwa katika kipindi cha miezi minne pekee. Je, Afrika inashindwa kukabili magonjwa yaliyopuuzwa?
Maoni: Juhudi za kusitisha mapigano nchini Ukraine
Rais wa Marekani, Donald Trump, aliahidi kuvimaliza vita hivyo mara tu baada ya kuingia madarakani
Mwangaza wa Ulaya: Juhudi za amani katika mzozo wa Ukraine
Viongozi wa ngazi za juu wa Urusi na Ukraine wanatarajiwa kukutana wiki hii mjini Instanbul nchini Uturuki, kujadili namna ya kuumaliza mzozo wao uliongia mwaka wa tatu na ambao unaendelea kusababisha maafa na uharibifu mkubwa. Ikiwa yatakuwepo, unadhani, kuna ishara zozote za kwamba mara hii mazungumzo hayo kati ya Urusi na Ukraine yatafanikiwa? Ungana na Bakari Ubena.
India na Pakistan zinapambana katika mzozo wa Kashmir
Kwa sasa hali si shwari kati ya India na Pakistan huku kukiwa na hofu ya watu zaidi kuuwawa.
Ufahamu ugonjwa wa Kala-azar, mojawapo ya maradhi yaliyobezwa Afrika
Idadi ya vifo kutokana na mlipuko wa ugonjwa wa Kala-azar nchini Kenya imefikia watu 33 na maambukizi zaidi ya elfu moja katika kipindi cha miezi 4, na bado yanaendelea. Mlipuko huu unatupa taswira ya mapambano ya Afrika na magonjwa yaliyopuuzwa, na vilevile athari yake kwa jamii. Sikiliza makala ya Afya Yako iliyoandaliwa na Wakio Mbogho.
Wakulima Kenya watumia AI kuboresha mbuzi wa maziwa
Akili Mnemba, AI, sasa inatumika kubaini mbinu bora za uzalishaji wa mifugo na kuongeza ufanisi katika shughuli za ufugaji. Wataalamu wanasema huu ni mwelekeo mpya unaoweza kubadilisha sekta ya ufugaji barani Afrika. Ni katika makala ya Sema Uvume na Wakio Mbogho.
AfD yainishwa kama kitisho cha demokraisa Ujerumani
Shirika la Ujerumani la ujasusi wa ndani limekiainisha rasmi chama cha AfD kuwa cha mrengo mkali na kukieleza kuwa tishio kwa taratibu za kidemokrasia nchini. Uamuzi huo unatoa mamlaka kwa idara husika ya kukimulika chama hicho ikiwa ni pamoja na kuwatumia makachero na mbinu zingine ili kukipeleleza.
Je, unakoroma sana usiku?
Unajikuta unaamka mchovu hata baada ya kulala usiku mzima? Unapumua kwa shida usingizini au kuamka ghafla ukikohoa? Ikiwa jibu ni ndiyo, kuna uwezekano mkubwa kuwa unakabiliwa na tatizo hatari la kiafya linalojulikana kama Obstructive Sleep Apnea—hali ambapo njia ya hewa huzibwa wakati wa usingizi bila wewe kujua!
Maoni Meza ya Duara: Siku 100 za Rais Trump Madarakani
Baada ya siku 100 madarakani, Rais Trump amesema miezi yake ya kwanza madarakani imekuwa na mafanikio makubwa lakini tathmini yake inatofautiana sana na mitazamo ya wataalamu na wachambuzi wengi ambao wameshangazwa na yale ambayo ameyafanya hadi sasa. Kwenye Maoni Meza ya Duara watachambuzi wanayajadili hayo. Mwenyekiti ni Zainab Aziz
Peter Magyar na harakati za kuukwaa Uwaziri Mkuu Hungary
Nchini Hungary, Peter Magyar ana ushawishi mkubwa wa kisiasa. Anaonekana kuwa tishio kwa utawala wa Viktor Orban. Kama mambo yatamwendea vyema, huenda akawa Waziri Mkuu ajaye baada ya uchaguzi utakaofanyika 2026. Kufahamu zaidi sikiliza makala haya ya Mwangaza wa Ulaya.
Makala ya Karibuni 26.04.2025
Mgeni wetu ni Mwanamuziki wa kizazi kipya Abuu Mnette, akitambulisha wimbo wake mpya "Tafuta Bwana."
Maoni: Miaka miwili tangu vita vya Sudan vilipoanza
Je suluhu inaweza kupatikana katika mgogoro wa nchini Sudan
Utamaduni wa Singo ya kisasa kwa maharusi Mombasa
Ujue utamaduni wa singo, desturi ya kale yenye mizizi ndani ya jamii za waswahili wa Pwani ya Afrika Mashariki, Kwa karne nyingi, kusingwa ilikuwa sehemu muhimu ya maandalizi ya bibi harusi. Fathiya Omar anayo mengi katika makala ya Utamaduni na Sanaa.
Wanaofanya kazi na AI wanavyohatarisha afya ya akili Kenya
Nyuma ya mapinduzi ya teknolojia ya akili mnemba yanayoonekana, kuna kikosi kazi kisichoonekana kinachoundwa na mamilioni ya wafanyakazi wanaoainisha na kutathmini taarifa kwa ajili ya kuilisha teknolojia hiyo.
Ulihimili vipi kishindo cha kuwachwa na mpenzi wako?
Katika kipindi cha vijana mubashara 77 asilimia, Suleiman Mwiru anajadiliana nawe kuhusu masuala ya mahusiano, na anakuuliza je umeshawahi kuacha au kuachwa na mpenzi wako na ulikimudu vipi kishindo hicho?
Ruge: Hatukai kwenye chama kisichowasikiliza wengine
Nchini Tanzania chama kikuu cha upinzani CHADEMA kinaonekana kimekumbwa na mpasuko kuhusu sera yao mpya ya "no reform no election" sehemu fulani ya wanachama inaonekana hawakubaliani na sera hiyo. Zaidi juu ya hilo, Mohammed Khelef amezungumza na aliyekuwa katibu wa masuala ya kijamii na kijinsia, Catherine Ruge.
Philo Tsoungui, mpiga ngoma wa kike Ujerumani
Makala ya Utamaduni na sanaa inamuagazia kwa undani Philo Tsoungui, mmoja wa wapigangoma maarufu zaidi wa kike nchini Ujerumani. Akitokea katika familia mchanganyiko, mama Mjerumani na Baba kutoka Kameruni, Philo, sio tu anapambana kuvuka vizuizi vya mfumo dume, bali pia changamoto za ubaguzi dhidi ya watu weusi.
Jukwaa la Manufaa
Sikiliza maoni yako msikilizaji katika kipindi cha Jukwaa la Manufaa, kilichoandaliwa na kuongozwa na Angela Mdungu. Kipindi hiki kinatoa nafasi kwa msikilizaji kusema kile kilicho moyoni mwake, kinachomkera na kinachomfurahisha. Kuna nafasi pia ya kuwasikia wanajukwaa wengine watakaotoa dukuduku lao kupitia njia ya simu.
Vipi kuishi na watoto wenye usonji ?
Ulimwengu unaadhimisha kila Aprili 2 siku ya Usonji. Ili kufahamu hasa watoto wenye usonji wanaweza kupewa malezi ya aina gani kukuza vipawa vyao, Rashid Tshilumba amezungumza na Eunice Njeru, kutoka Nakuru, Kenya, yeye ana mtoto mwenye usonji na kwanza anaeleza tofauti iliyopo kati yake na watoto wengine.
Jukwaa la Manufaa
Sikiliza maoni yako msikilizaji katika kipindi cha Jukwaa la Manufaa, kilichoandaliwa na kuongozwa Angela Mdungu. Kumbuka katika kipindi hiki tunatoa nafasi ya msikilizaji kusema kile kilicho moyoni mwako, kinachomkera na kinachomfurahisha. Kuna nafasi pia ya kuwasikia wanajukwaa wengine watakaotoa dukuduku lao kupitia njia ya simu.
Namna akili mnemba inavyotambua na kukabiliana na ufisadi
Teknolojia ya akili mnemba yaani (AI) imeleta mageuzi kwenye nyanja mbalimbali, ikiwemo kwenye sekta ya utawala na uadilifu wa serikali. Kwa kutumia uwezo wake wa kuchambua data kubwa kwa haraka na kwa usahihi, akili mnemba imekuwa nyenzo muhimu kwa serikali katika ufuatiliaji, na kuzuia vitendo vya ufisadi.
Uhusika wa wanawake katika uongozi wa kisiasa Uganda
Kuelekea uchaguzi mkuu ujao nchini Uganda mwaka 2026, wanawake wamejitokeza na ilani yao ambayo wangependa izingatiwe na vyama vyote vya siasa ili kuhakikisha masuala yao muhimu yanapewa kipaumbele kuwawezesha kushiriki ipasavyo katika siasa, utawala na uchumi wa nchi.
Wanawake watengeneza dawa za kuua mbu nchini Kenya
Makala ya Wanawake na Maendeleo inalimulika kundi la wanawake wa nchini Kenya walioungana kuzalisha dawa ya mbu.
Makala yetu leo: Utalii katika mwezi wa Ramadhan Zanzibar
Wakati wa mwezi Mtukufu wa Ramadhani maisha hubabadilika Zanzibar! Biashara nyingi hupunguza shughuli mchana, mikahawa hufungwa, na wenyeji hujikita katika ibada. Lakini vipi kuhusu sekta ya utalii? Wageni wanafanya marekebisho gani wanapowasili hapa? Fuatana na Salma Said, akiangazia jinsi utalii na Ramadhani vinavyoingiliana Zanzibar!
Mtu na Mazingira: Tanzania na mradi wa Kijani Hai
Ili kukabiliana na uharibifu wa mazingira nchini Tanzania, Wizara ya Kilimo kwa kushirikiana na Ofisi ya Makamu wa Rais na Shirika la Maendeleo la Ujerumani (GIZ), wameanzisha Mradi wa Kijani Hai. Kijani Hai ni mpango ulioanzishwa 2017 nchini Tanzania na unaolenga uhifadhi wa mazingira, upandaji miti, na kuhamasisha matumizi endelevu ya rasilimali asili.
Afya Yako: Tiba za kisasa za kupambana na maradhi ya TB
Kwa mujibu wa Shirika la Afya Duniani, WHO mwaka 2023, watu milioni 1.25 walifariki kutokana na kuugua kifua kikuu (TB), wakiwemo 161,000 waliokuwa na Virusi Vya Ukimwi. WHO inaonya kuwa kupungua kwa ufadhili wa afya duniani kunahatarisha mafanikio haya. Ungana na Fathiya Omar, makala ya Afya yako.
Maoni: Hofu ya kuzuka mgogoro mwingine nchini Sudan Kusini
Kwenye kipindi cha Maoni Meza ya Duara, wachambuzi wetu wanaijadili Sudan Kusini. Mkataba wa Amani wa mwaka 2020 uliiimarisha serikali ya mseto ya rais Salva Kiir na makamu wake wa kwanza Riek Machar lakini huo haukuwa mwarobaini kamili kwa sababu nchi hiyo haijawahi kuwa tulivu. Jee! kwa nini Sudan Kusini mara kwa mara inarudi pale pale, kwenye migogoro? Mwenyekiti ni Zainab Aziz
Jukwaa la manufaa
Sikiliza maoni yako msikilizaji katika kipindi cha Jukwaa la Manufaa, kilichoandaliwa na kuongozwa Angela Mdungu
Meza ya Duara: Je, Raila ni bingwa wa miafaka au msaliti?
Mwanasiasa mashuhuri wa upinzani nchini Kenya, Raila Odinga, ameingia kwenye muafaka mwengine wa kisiasa na mahasimu wake. Safari hii ikiwa ya nne, amesaini muafaka na Rais William Ruto, baada ya huko nyuma kuingia kwenye miafaka kama hiyo na Rais Daniel arap Moi, Rais Mwai Kibaki na Rais Uhuru Kenyatta.
Makala ya Afrika Wiki Hii
Mzozo wa Jamhuri ya kidemokrasia ya Kongo unazidi kutanuka, Jumuiya ya SADC imeamua kuondoa wanajeshi wake mashariki mwa nchi hiyo. Kando na hilo, baada ya rais wa Kenya William Ruto na Waziri Mkuu wa zamani Raila Odinga kutia saini mkataba wa kufanya kazi pamoja, wakenya wasema Odinga ameweka mbele masilahi yake na sio ya taifa. Amina Abubakar ana mengi katika Makala ya Afrika Wiki Hii.
Uraibu wa matumizi ya spika za masikio kwa vijana
Maendeleo ya teknolojia na upatikanaji rahisi wa vifaa vya kielektroniki umewapa sababu vijana ya kutumia spika za masikio kwa kiwango ambacho kinaleta hofu kwa wataalamu wa afya, baadhi ya vijana wanasema wanasikiliza kwa saa zaidi ya saba kwa siku huku sauti ikiwa juu.
Usalama wa miundombinu ya gesi na changamoto zake
Tanzania imekuwa ikifanya utafiti kuhusu ugunduzi wa gesi asilia kwa zaidi ya miaka hamsini, na ugunduzi wa kwanza ulifanyika mwaka 1974 katika kisiwa cha Songosongo mkoani Lindi na baadaye mkoani Mtwara. Lakini usalama wa miundombinu ya gesi na changamoto zake kwa mazingira ni zipi?
Matarajio ya CHADEMA kuelekea uchaguzi Mkuu
Tanzania inajiweka sawa kuingia kwenye uchaguzi Mkuu hapo baadae mwaka huu, katikati hayo upo mgawanyiko, wapo ambao wanataka mabadiliko ya katiba kabla ya kuingia kwenye mchakato huo wa kidemokrasia lakini wapo wanaona muhimu kufanyika uchaguzi kwanza.
Vijana na mitindo isiyojali jinsia
Kumekuwepo na mabadiliko makubwa kwenye mitindo ya uvaaji kote ulimwenguni. Katika nyakati hizi huwezi kushangaa kumuona msichana amevaa pengine raba ambazo pia anavaa mwanaume, na kwa upande wa wanaume pia huwa ni hivyohivyo. Je, nini kimesababisha hali hii, na je wewe ni mmoja wapo? Karibu usikilize makala hii ya Vijana Mchakamchaka, usikie wenzako wanasemaje?
Je, zipo faida za kufanyakazi siku nne kwa wiki?
Ujerumani imefanya majaribio ya wafanyakazi kufanya kazi kwa siku nne badala ya tano kwa wiki kwa malipo ya mshahara ule ule,lengo ni kumpa nafasi mtu kuwa na muda wa ziada kwa mambo mengine ikiwemo familia. Hebu sikiliza kwa undani.
Kabendera na Kitabu "In the name of President"
Mwanahabari aliyepitia panda shuka nyingi ikiwemo kuwekwa kizuizini na kushikiliwa kwa hati zake za kusafiria Erick Kabendera amefanya mazungumzo na Sudi Mnette akieleza kilichomsukuma kuandika kitabu hicho.
Utamaduni wa manukato na asili yake kwa waswahili
Kwa utamaduni wa kiswahili udi ama manukato ni sehemu ya urembo wa usali ukitambulika kwa harufu yake ya kufutia ikidumu mwilini na kwenye nguo kwa muda mrefu. Lakini unajua asili yake? Sikiliza makala
Makala ya Afrika Wiki Hii
Mzozo wa Mashariki mwa Kongo unaendelea kufukuta. Mkutano wa viongozi wa Afrika wafanyika Addis Ababa Ethiopia, ajenda kuu ni mzozo wa DRC, lakini nafasi ya kufanikiwa juhudi za kidiplomasia za kuutatua mzozo huo ni ndogo, je ni kwanini? Kwa haya na mengine mengi sikiliza Afrika wiki hii na Amina Abubakar.
Matumaini mapya yachomoza Sudan
Sudan inataka kuweka msingi wa kurejea kwa utawala wa kiraia katika mpango unaojumuisha kuundwa kwa serikali ya mpito, kumteua waziri mkuu wa kiraia na kuanzisha mdahalo wa kitaifa na vyama vya siasa na asasi za kiraia. Jiunge na Josephat Charo katika kipindi cha Maoni mbele ya Meza ya Duara.
Vijana wanavutiwa na uhuru wakiwa kazini
Maendeleo ya teknolojia yamewapa vijana nafasi kubwa ya kufanyakazi katika mazingira huru, huku ofisi nyingi zikivutiwa na mtindo huo kutokana na kupunguza gharama za uendeshaji ofisi. Katika makala ya Vijana Mchakamchaka hilo ndio vijana wanajadili linafaida kwao?
DeepSeek Akili Mnemba iliyoteka soko la teknolojia
DeepSeek imeleta mapinduzi katika mukhtadha wa teknolojia ya Akili Mnemba kutokana na namna ambavyo inachakata taarifa zake, lakini upo wasiwasi wa namna inachakata data zake, wataalamu wanaonya kuwa inaweza kutumiwa vibaya katika kutoa taarifa.
Matetemeko ya ardhi yasababisha hofu nchini Ugiriki
Tangu mwanzoni mwa mwezi Februari kumeshuhudiwa mkururo wa matetemeko ya ardhi nchini Ugiriki hasa katika kiswa cha Santorini na kuzusha hofu kulipuka kwa volkano katika siku za usoni. Makala ya Mwanza wa Ulaya inatuama hapo nahodha ni Bakari Ubena
Ukurasa uliotangulia
Ukurasa 2 wa 6
Ukurasa unaofuatia