You need to enable JavaScript to run this app.
Nenda kwenye maudhui
Nenda kwenye orodha kuu
Nenda tovuti zaidi za DW
Vidio zetu
Sauti zetu
Maeneo
Tanzania
Kenya
Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo
Afrika
Ulaya
Mada
Haki za binadamu
Mazingira
Afya
Teknolojia
Kategoria
Matukio ya Kisiasa
Masuala ya Jamii
Michezo
Yanayoangaziwa
Mzozo wa Kongo Mashariki
Mzozo wa Israel na Hamas
Bundesliga
Sauti zetu
Vidio zetu
Matangazo
Picha: Zoonar/picture alliance
Makala zetu
Sikiliza makala kemkem tulizokuandalia
Ruka sehemu inayofuata Maudhui yote kwenye mada hii
Maudhui yote kwenye mada hii
Njia za kukabiliana na hofu ya kujifungua kwa mara ya kwanza
Kwa wanaojifungua kwa mara ya kwanza wakati mwengine wanakuwa na hofu kubwa ya kupitia mchakato mzima wa kujifungua. Wengi wanakuwa na uwoga baaada ya kuwasikia wanawake wengine wakizungumzia mchakato huo wa uzazi. Makala ya Afya Yako inakueleza njia za kukabiliana na hofu hiyo.
Ngoma za Njuga na jinsi zinavyorithishwa kupitia sanaa
Ngoma za Njuga ni aina ya ngoma za asili zinazochezwa kwa kuvaa njuga miguuni au mikononi, zikitamba kwa sauti ya kipekee inayochochea furaha, heshima na mdundo wa kuvutia. Alex mchovu anakupa umuhimu wa ngoma hizo na jinsi ya kuendeleza na kurithisha mila na tamaduni kupitia vipengele vya sanaa.
Makala ya Afrika Wiki Hii
Joto la kisiasa Tanzania linaendelea kupanda kuelekea uchaguzi mkuu wa Oktoba 29. Rais anaetetea kiti chake, Samia Suluhu Hassan, haonekani kuwa na mtihani mkubwa sana kwa kuwa vyama vikuu viwili vya upinzani hadi sasa havina wagombea. Katika Jamhuri ya kidemokrasia ya Kongo Jeshi bado linapambana na makundi ya wanamgambo na Morocco ndio mabingwa wa mashindano ya Kombe la CHAN-2024
Mkwamo wa soka la Wanawake visiwani Zanzibar
Soka la wanawake Zanzibar linakumbwa na changamoto kadhaa zinazozuia ukuaji wake licha ya vipaji vilivyopo visiwani humo. Hali ya uwekezaji duni imeathiri pakubwa ustawi wa wachezaji, uwepo wa viwanja vichache na ukosefu wa udhamini wa kutosha kwa timu za wanawake. Najjat Omar anaangazia hali ya soka la wanawake Zanzibar.
Mwelekeo wa magari ya umeme EVs nchini Kenya
Magari ya umeme nchini Kenya yanaanza kuchukua nafasi kubwa katika sekta ya usafiri huku juhudi za serikali na kampuni binafsi zikichochea mabadiliko kuelekea nishati jadidifu. Hata hivyo kuna wasiwasi miongoni mwa madereva kuhusu upatikanaji wa miundombinu ya kuchaji, hasa nje ya miji mikuu. Makala ya Sema Uvume yanaangazia hamasa ya kuendana na mabadiliko ya kidijitali nchini Kenya.
Zanzibar - Kisiwa maarufu cha viungo duniani
Zanzibar inasifika kwa uwepo wa mashamba ya viungo ambapo wageni hujifunza kuhusu karafuu, mdalasini, vanila na viungo vyingine vinavyokifanya kisiwa hicho kuwa kitovu cha biashara ya viungo kimataifa. Viungo hivyo hutumika katika tiba, mapishi na ni mojawapo ya utamaduni wa jadi visiwani Zanzibar. Makala ya Utamaduni na Sanaa inamulika jumba la makumbusho la viungo visiwani humo.
Utamaduni wa jamii ya Wasuba nchini Kenya
Jamii ya Wasuba nchini Kenya ni mojawapo ya makabila ya asili yaliyo na historia ya kipekee na tamaduni tajiri, ingawa kwa sasa jamii hiyo inakabiliwa na changamoto ya kutambuliwa na kuhifadhi utambulisho wao wa kitamaduni. Kwenye Makala ya Utamaduni na Sanaa, Musa Naviye anaiangazia jamii ya Wasuba wanaojitambulisha pia kama Abasuba.
Jukwaa la manufaa
Yasikie maoni uliyotutumia msikilizaji yakijumuisha kero, ushauri na hata pongezi kuhusu masuala kadha wa kadha yanayoendelea kwenye jamii yako kupitia Jukwaa la Manufaa. Ungana naye Angela Mdungu kwa takriban dakika tisa za kipindi hiki akiyapeperusha hewani maoni yako.
Afrika wiki hii
Nchini Tanzania kesi dhidi ya Mwenyekiti wa CHADEMA Tundu Lissu imepelekwa Mahakama kuu+++Wabunge nchini Kenya waghadhabishwa na madai ya Rais William Ruto kwamba baadhi yao huchukua hongo ili kupitisha miswada bungeni+++ Amnesty International yashutumu makundi ya waasi na makundi yanaoshirikiana na jeshi la Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo kwa ukatili dhidi ya wanawake na mauaji holela ya raia.
Programu inayotumia Akili Mnemba kutafsiri lugha ya alama
Kampuni moja ya nchini Kenya inafanya juhudi za kutafsiri maneno kwenda katika lugha ya alama kwa kutumia picha za kielektroniki zinazofahamika kama Avatar. Ungana na Angela Mdungu katika makala ya Sema Uvume kufahamu zaidi.
Utata kuhusu kura ya mapema Zanzibar
Tume ya Uchaguzi Zanzibar (ZEC) imesema, kura ya mapema itafanyika kama ilivyo kwenye sheria ya tume hiyo licha ya chama kikuu cha upinzani- ACT Wazalendo kupinga. Mohammed Khelef amezungumza na Ismail Jussa makamu mwenyekiti wa chama hicho kujua ni kwanini wanalipinga hilo.
Je dunia inafanya vya kutosha kulinda uhuru wa kuabudu?
Siku ya kumbukumbu ya waathirika wa ukatili wa kidini ni siku inayowakumbuka wale wote walioteseka, kujeruhiwa au kupoteza maisha kwasababu ya imani zao. Siku hii pia inaibua masuali mazito ya iwapo dunia inafanya juhudi za kutosha kulinda uhuru wa kuabudu. Mbiu ya Myonge inaangazia hilo, mtayarishaji ni Najjat Omar.
Changamoto za vijana kufikia soka ya kulipwa
Katika sabini na saba asilimia tunakuuliza, je, ni changamoto gani zinazowakabili vijana wa mashinani katika azma yao ya kutaka kufikia kiwango cha kuwa wachezaji wa kulipwa? Jacob Safari ameyaangazia hayo na mengi katika Makala ya Vijana Mubashara.
Wamassai waendeleza mila kupitia sanaa ya muziki, Kajiado
Jamii ya Wamassai nchini Kenya imekuwa ikijivunia mila zake za jadi kwa muda mrefu ila ujio wa kizazi kipya cha vijana kutoka jamii hiyo, imeonekana kama isiyozingatia desturi zao. Ndio maana viongozi wa jamii hiyo wanaendesha sasa kampeni ya kuwafunza vijana mila na desturi zao kupitia sanaa ya muziki. Makala ya Utamaduni na Sanaa inaangazia hayo.
Kenya yatoa mafunzo ya magari ya umeme kwa madereva wake
Licha ya wamiliki wa magari binafsi Kenya kuzidi kununua magari ya umeme, bado nchi hiyo haina magari ya aina hiyo katika sekta ya usafiri wa umma. Baadhi ya wadau wamezindua mpango wa mafunzo wa magari hayo, unaolwaenga madereva wa usafiri wa umma, wakihimiza matumizi yake yana faida nyingi.
Je teknolojia ya AI inaweza kukupa ushauri wa kimapenzi?
Katika makala ya vijana Mubashara tunakuuliza je, kwanini baadhi ya vijana wameamua kugeukia teknolojia ya akili mnemba ama AI kwa ajili ya kupata ushauri wa kimapenzi na hata kuanzisha mahusiano, ukizingatia kuwa AI haina hisia kama alivyo mwanadamu?
Makala ya Afrika wiki hii
Hatua ya matifa kadhaa ya Afrika kukubali kuwapokea wahamiaji waliofukuzwa kutoka Marekani imeibua hisia mseto na wasiwasi wa kiusalama. Nchini Tanzania, mchakato wa uteuzi wa viongozi watakaochuana katika uchaguzi mkuu ujao ulishika kasi huku vyama vya upinzani vikiwachagua wagombea wao wa kiti cha urais. Na mzozo wa mashariki mwa DRC waendelea kufukuta licha ya makubaliano ya amani.
Maoni: Miaka 80 ya mashambulizi ya Hiroshima na Nagasaki
Watu wa Japan na wa dunia nzima kwa jumla wanayakumbuka maafa makubwa yaliyotukia kwenye miji ya Japan ya Hiroshima na Nagasaki miaka 80 iliyopita. Marekani iliishambulia miji hiyo kwa mabomu ya nyuklia. Wachambuzi wanajadili matumizi hasi na chanya ya tekinolojia ya nyuklia. Mwenyekiti Zainab Aziz
Wodi ya tumaini kwa watoto njiti
Watoto wanaozaliwa kabla ya muda yaani watoto Njiti wanaelezwa kukabiliwa na changamoto mbalimbali ikiwemo ya kukosa kunyonya maziwa ya mama kutokana na sababu mbalimbali ikiwemo ya kuwapoteza mama zao wakati wa uzazi. Tanzania inaelezwa kushika nafasi ya 12 kwa nchi zenye idadi kubwa ya watoto Njiti duniani. Sikiliza makala hii ya Afya Yako na Anuary Mkama. #DW Kiswahili
Uhifadhi wa mti wa shea ni biashara nyeti nchini Uganda
Mti wa shea ni muhimu sana si tu kwa uhifadhi wa mazingira katika ukanda kati ya Uganda na Ghana barani Afrika lakini pia kama kitega uchumi nyeti kwa jamii zinazoishi maeneo hayo. Tukichukua mfano wa Kaskazini mwa Uganda, mti huo pamoja na mazao yake umekuja kuthaminiwa sana baada ya watu kufahamu manufaa yake endelevu kwa maisha yao badala ya wao kuikata kwa ajili ya mkaa na kuni.
Njuga zacheza utaifa na mshikamano nchini Tanzania
Katika jamii nyingi za Kiafrika, sanaa na utamaduni ni roho ya watu,ni urithi usiogusika unaounganisha vizazi, unaofundisha maadili na kuendeleza mshikamano wa kijamii. Leo, tunamulika ngoma za njuga aina ya ngoma za asili zinazochezwa kwa kuvaa njuga miguuni au mikononi. Kupitia #DW sikiliza makala hii ya Utamaduni na Sanaa na Alex Mchomvu.
Mwangaza wa Ulaya: Utalii wa kupindukia katika miji ya Ulaya
Utalii wa kupindukia umekuwa tatizo linaloongezeka katika miji mingi na maeneo ya likizo barani Ulaya. Hilo limekuwa changamoto kubwa kwa wakazi wanaolalamika kukosa nafasi zenye utulivu, kupanda kwa bei ya makazi, chakula na bidhaa nyingine muhimu. Baadhi ya nchi sasa zimeanza kuchukua hatua za moja kwa moja kudhibiti mtiririko wa wageni kwa kuweka kodi ya utalii na kuanzisha kikosi maalum.
Pica: Tatizo la kiafya la kula vitu visivyo chakula
Afya Yako wiki hii inaumulika ugonjwa wa Pica unaosababisha mtu kupenda kula vitu visivyo chakula.
Visa vya ukeketaji vyaongezeka kaunti ya Marsabit
Ripoti ya hivi karibuni imebainisha kuwa ukeketaji na ndoa za mapema zimeongezeka katika kaunti ya Marsabit nchini Kenya. Visa hivyo vinaripotiwa licha ya mamlaka nchini humo kupiga marufuku ukeketaji huku wakaazi wengi wakieleza wasiwasi kuhusu ongezeko hilo na kuhimiza hatua madhubuti kuchukuliwa kuzuia visa hivyo. Mtayarishaji wa Makala Yetu Leo ni Michael Kwena.
Wafanyakazi Ujerumani wakabiliwa na maisha ya mashaka
Wafanyakazi kadhaa nchini Ujerumani wanakabiliwa na hali ngumu ya maisha huku wakishindwa kumudu kodi za nyumba licha ya kuwa na ajira. Nyumba za kupanga ni vigumu kuzipata na bei yake ni kubwa, hasa kwenye miji kama Berlin na hivyo sio rahisi kwa watu wenye vipato vya chini kumudu kodi za mijini. Mtayarishaji wa Makala ya Sura ya Ujerumani ni Zainab Aziz.
Kenya yahamasisha wanafunzi kujiunga na masomo ya teknolojia
Kenya inaendeleza juhudi za kuwahamasisha wanafunzi kujiunga na masomo ya Sayansi, Teknolojia, Uhandisi na Hisabati - maarufu kama STEM. Shirika la Anga la Kenya (KSA) limeanzisha mpango maalum kwa shule za upili kuchangia katika kampeni hii. Makala ya leo ya Sema Uvume inamulika mada hiyo.
Ugunduzi wa Kifaa cha kuonya kutokea kwa tetemeko la ardhi
Mara nyingi utatuzi wa matatizo katika jamii ndio chachu ya kubuniwa kwa programu tofauti za kiteknolojia ili kuwasaidia wahitaji. Ugunduzi wa teknolojia mpya una nafasi ya kuleta faida kijamii, kiuchumi, kimazingira na mambo mengineyo.
Jukwaa la Manufaa
Jukwaa la manufaa la DW Kiswahili linakupa fursa ya kutoa kero, pongezi au ushauri juu ya masuala mbalimbali ya jamii. Bila kusahau kuna burudani ya muziki itakayoyasindikiza maoni yako.
Kifaa maalumu kinachotumia App kuonesha Makka ilipo
Hivi karibuni yalifanyika maonesho maalum ya wajasiriamali wa teknolojia wa Kiislamu jijini London nchini Uingereza. Moja ya vitu vilivyowavutia washiriki wengi katika maonesho hayo ni kifaa kinachosaidia kutambua Makka ilipo na mswala wa kidijitali maalum kwa kufanyia sala.
Mpango wa 'Elimu haina mwisho' kwa wasichana
Elimu haina mwisho, ni mradi maalum wa kuwasaidia wasichana Tanzania, ambao hawajamaliza kidato cha nne, waliositisha masomo kwa sababu mbalimbali, ikiwemo ya kupata ujauzito, ufukara ndani ya familia au kuugua kwa muda mrefu. Mradi huu unaratibiwa na Wizara ya Elimu nchini humo.
Maoni Siasa za Tanzania kuelekea uchaguzi - MP3-Stereo
Chama tawala cha CCM kilichopo madarakani kwa muda wote, kinawania kuendelea kusalia madarakani
Kenya yaanzisha kampeni ya chanjo za watoto
Kenya imezindua kampeni ya siku 10 ya kuchanja watoto dhidi ya ukambi, rubela na homa ya matumbo. Watoto walio katika hatari ya kuugua ni wale walio chini ya miaka mitano na ndio hao serikali inaowalenga katika kutoa chanjo. Thelma Mwadzaya anaangia mengi juu ya chanjo hiyo katika makala hii ya Afya yako.
Je upinzani Uganda utaweza kuungana kumng'oa Museveni?
Kuelekea uchaguzi mkuu wa mwaka 2026 uganda, vyama vya upinzani vimeanza harakati za kujiimarisha kwa kufanya mashauriano ya kuungana, huku baadhi ya wanachama waliokata tamaa na uongozi wa vyama vikuu wakianzisha vyama vipya. Hata hivyo, wachambuzi wa siasa wanaona nafasi ya upinzani ikizidi kudhoofika.
Nini kinasababisha mdondoko wa elimu Mtwara?
Mkoa wa Mtwara uliopo Kusini Mashariki mwa Tanzania ni miongoni mwa mikoa inyokabiliwa na changamoto ya elimu. Vijana tugutuke inaangazia athari za mdondoko wa elimu katika mkoa huo na tunauliza je, nini kinasababisha changamoto hiyo?
Afrika: Miradi ya kukabiliana na tabianchi itekelezwe
Mshauri wa Rais wa Tanzania katika masuala ya mabadiliko ya tabianchi Richard Muyungi ambaye pia anawakilisha mataifa ya Afrika katika masuala ya mazingira Umoja wa Mataifa amesema njia pekee ya kukabiliana na mabadiliko ya tabianchi ni utekelezaji wa miradi ya kukabiliana na kadhia hiyo kikamilifu.
Kenya kujikita katika teknolojia ya anga kupitia AI
Kenya imeanza kulea vipawa vya wanafunzi ambao wanapenda taaluma ya anga kwa kutumia teknolojia ya kisasa ya Akili Mnemba AI. Mpango huu haulengi tu mafanikio ya kisayansi bali pia lukuza kizazi kipya katika fani ya anga.
Denmark: Tutarejesha ushawishi wa Ulaya Kimataifa
Denmark imechukua uenyekiti wa Umoja wa Ulaya kwa kipindi cha miezi sita, Ukraine ni sehemu ya kipaumbele chake katika wakati huu, huku ikisisitiza kuwa itafanya juu chini katika kurejesha ushawishi wa Ulaya kimataifa.
Unaujua upishi wa visinia?
Makala ya Wanawake na Maendeleo inaangazia juhudi za mwanamke aitwaye Flora Kiunzi, aliyethubutu kuacha kazi benki na kugeukia upishi na hasa ule wa visinia mkoani Mtwara, Tanzania. Salma Mkalibala alizungumza nae.
Kampeni ya kidijitali dhidi ya GBV yazindulia Kenya
Kenya imezindua kampeni ya kidijitali dhidi ya unyanyasaji wa kijinsia ambayo ni juhudi ya kukabiliana na ongezeko la unyanyasaji dhidi ya wanawake na wasichana kupitia mbinu bunifu, zinazoendeshwa na teknolojia.
Jukwaa la Manufaa
Jukwaa la manufaa la DW Kiswahili linakupa fursa ya kutoa kero, pongezi au ushauri juu ya masuala mbalimbali ya jamii. Bila kusahau kuna burudani ya muziki itakayoyasindikiza maoni yako.
Makala ya Karibuni 29.06.2025
Katika kipindi "Karibuni" awamu mpya wa michezo ya Noa Bongo Jenga Maisha Yako imeanza kurekodiwa jijini Dar es Salaam.
Muziki wa Hip hop ni sauti mbadala wa jukwaa la siasa?
Katika makala ya vijana mubasharana tunakuuliza muziki wa Hip Hop ni sauti ya mtaa — unaopaza kilio cha wanyonge, ukihoji mfumo, na kudai mabadiliko, ama umegeuka biashara ya burudani na kupoteza asili yake?
Wanawake wa Burundi bado ni wachache uongozini
Ushiriki wa wanawake katika taasisi za utawala na miradi ya ujasiriamali bado ni mdogo nchini Burundi. Mkuu wa kitengo cha mikopo ya miradi ya ujasiriamali anasema kati ya miradi 4,700 waliyopokea tangu 2021, miradi 700 ndio ilikuwa ya wanawake. Wizara ya mshikamano kitaifa imehimiza wanawake kujitokeza kupiga kura na kuwania uongozi kwenye uchaguzi wa mwezi Julai. Amida ISSA alituandalia ripoti.
Jukwaa la Manufaa
Jukwaa la manufaa la DW Kiswahili linakupa fursa ya kutoa kero, pongezi au ushauri juu ya masuala mbalimbali ya jamii. Bila kusahau kuna burudani ya muziki itakayoyasindikiza maoni yako. Ungana na Angela Mdungu akupandishe jukwaani.
Makala ya Afrika wiki hii
Sekeseke la maandamano laikumba Kenya kufuatia sakata la kifo cha utata cha mwanablogu,Albert Ojwang,polisi yatowa taarifa ya mkanganyiko. Bajeti za mataifa ya Afrika Mashariki kwa mwaka 2025/26 zawasilishwa. Mafuriko yasababisha maafa makubwa Afrika Kusini na Chama tawala Burundi CNDD-FDD chatwaa ushindi uchaguzi wa bunge na madiwani. Jiunge na Saumu Mwasimba
Kuzagaa kwa taka Dar es Salaam, Tanzania
Isikilize makala ya Mtu na Mazingira ambayo leo inaangazia changamoto ya kuzagaa kwa taka huko Dar es Salaam, Tanzania na jinsi ya kukabiliana na changamoto hiyo ambayo imekuwa kero kwa wakaazi wa mji huo. Anuary Mkama ndiye aliyeiandaa makala hii.
Kuhifadhi utamaduni usioshikika
Serikali ya Tanzania kwa ushirikiano na Shirika la Umoja wa Mataifa la Elimu, Utamaduni na Sayansi, UNESCO, imeanza kuandaa mchakato wa kuhifadhi utamaduni usioshikika. Mfumo huo unalenga kuhifadhi, nyimbo, ngoma, asili za jadi miongoni mwa mambo mengine. Msikilize Alex Mchomvu katika makala hii ya utamaduni na sanaa.
Mpishi wa Visinia aliyeacha kazi benki
Sikiliza makala ya wanawake na maendeleo inayomuangazia mwanamke aliyethubutu kuacha kazi benki na kugeukia upishi hasa wa visinia katika mkoa wa Mtwara huko Tanzania. Salma Mkalibala ndiye aliyeandaa makala hii.
Maoni: Rwanda yajiondoa kutoka kwenye Jumuiya ya ECCAS
Wiki hii kwenye Maoni Meza ya Duara watalaamu wanaujadili uamuzi wa Rwanda wa kujiondoa kutoka kwenye Jumuiya ya Kiuchumi ya nchi za Afrika ya Kati, ECCAS, baada ya viongozi wa nchi za jumuiya hiyo kuamua kuurefusha urais wa zamu wa Guinea ya Ikweta na kuinyima Rwanda kuchukua nafasi ya uenyekiti wa zamu. Mwenyekiti ni Zainab Aziz
Chama kipya cha Gachagua kitashawishi vipi siasa za Kenya?
Aliyekuwa, naibu wa rais wa Kenya, ambaye hivi sasa ni kiongozi mkuu wa chama cha Democracy for Citizens Party (DCP), Rigathi Gachagua, ameendelea kuimarisha safari zake za kampeni kukinadi chama chake kipya. Je, chama hiki kipya kitakuwa kikubwa kiasi gani kuweza kuwa na ushawishi katika siasa za Kenya kuelekea uchaguzi mkuu ujao? Jiunge na Josephat Charo katika kipindi cha Maombi mbele ya Duara.
Ukurasa uliotangulia
Ukurasa 1 wa 6
Ukurasa unaofuatia