Wakati wa mwezi Mtukufu wa Ramadhani maisha hubabadilika Zanzibar! Biashara nyingi hupunguza shughuli mchana, mikahawa hufungwa, na wenyeji hujikita katika ibada. Lakini vipi kuhusu sekta ya utalii? Wageni wanafanya marekebisho gani wanapowasili hapa? Fuatana na Salma Said, akiangazia jinsi utalii na Ramadhani vinavyoingiliana Zanzibar!