Taarifa ya kujiuzulu kwa aliyekuwa balozi wa Tanzania nchini Cuba Humphrey Polepole, kesi ya Kiongozi Mkuu wa Upinzani Chadema Tundu Lissu na kuzinduliwa kwa dira ya maendeleo kwa miaka 25 ijayo ndizo taarifa kuu zilizovuma Tanzania. Mbabe wa siku nyingi wa vita nchini DRC Thomas Lubanga alikosoa mchakato wa mazungumzo kati ya serikali na M23 huku akitishia kuanzisha tena mapambano ya kijeshi.