Wanaharakati wa Kenya na Uganda, Boniface Mwangi na Agatha Atuahire waachiwa huru wakiwa hali dhaifu baada ya kushikiliwa siku kadhaa na maafisa wa usalama wa Tanzania. Rais wa zamani wa DRC Joseph Kabila aondolewa kinga ya kushtakiwa huku akituhumiwa kwa uhaini na serikali. Na ziara ya rais Cyria Ramaphosa Afrika Kusini pia ni sehemu ya yaliyoangaziwa barani Afrika wiki hii.