Mzozo wa Jamhuri ya kidemokrasia ya Kongo unazidi kutanuka, Jumuiya ya SADC imeamua kuondoa wanajeshi wake mashariki mwa nchi hiyo. Kando na hilo, baada ya rais wa Kenya William Ruto na Waziri Mkuu wa zamani Raila Odinga kutia saini mkataba wa kufanya kazi pamoja, wakenya wasema Odinga ameweka mbele masilahi yake na sio ya taifa. Amina Abubakar ana mengi katika Makala ya Afrika Wiki Hii.