Mazungumzo ya nyuklia ya Iran na Marekani kufanyika Muscat
12 Aprili 2025Matangazo
Wawakilishi hao watajadiliana kwa faragha 12.04.2025 katika mji mkuu wa Oman Muscat unaotumiwa mara kwa mara kwa usuluhishi kati ya Iran na nchi za Magharibi.
Soma zaidi: Rais wa Marekani atangaza mpango wa mazungumzo ya moja kwa moja ya nyuklia na Iran
Majadiliano hayo yanafanyika wakati Rais wa Marekani Donald Trump akisema Iran haiwezi kuwa na silaha za nyuklia na ametishia kuchukua hatua za kijeshi dhidi ya Iran kama makubaliano mapya hayatapatikana kwenye mazungumzo hayo.
Kwa upande wake, Waziri wa mambo ya nje wa Iran amesema inachotaka nchi yake ni kupata makubaliano ya haki na kweli katika majadiliano hayo.