Israel: Uhusiano wetu na Ujerumani umeingia doa
12 Agosti 2025Matangazo
Amesema mahusiano yao bado hayajavunjika, lakini yameingia doa.
Balozi huyo wa Israel amesema badala ya Ujerumani kujadili namna ya kuwapokonya Hamas silaha inajadili namna ya kuipunguzia silaha Israel akisisitiza kuwa uamuzi huo umelifurahisha kundi hilo la wanamgambo.
Ujerumani yasitisha mauzo ya silaha kwa Israel
Wiki iliyopita Kansela wa Ujerumani Friedrich Merz alitangaza kuwa nchi yake haitopeleka silaha Israel kwa kuhofia kuwa huenda zikatumika kwenye Ukanda wa Gaza.
Merz alisema uamuzi wake pia unatokana na mpango wa Israel kutaka kuidhibiti kikamilifu Gaza.
Baraza la Ulaya nalo pia limeyataka mataifa mengine wanachama wa Umoja wa Ulaya kuchukuwa hatua kama ya Ujerumani.