SiasaIsrael
Mahakama yaahirisha kesi ya ufisadi dhidi ya Netanyahu
29 Juni 2025Matangazo
Uamuzi huo wa mahakama unafuatia ombi la kiongozi huyo aliyetoa sababu za kuhitaji muda kushughulikia masuala ya kiusalama na kidiplomasia.
Haikuwa wazi iwapo chapisho la Rais wa Marekani Donald Trump kwenye mitandao ya kijamii limeshawishi uamuzi huo wa Mahakama. Trump alisema kesi hiyo inaweza kuvuruga uwezo wa Netanyahu kushiriki kikamilifu kwenye mazungumzo na kundi la Hamas pamoja na Iran.
Siku ya Ijumaa, Mahakama hiyo ilitupilia mbali ombi la wakili wa Netanyahu kuhusu kuahirisha keshi hiyo ikisema lilikuwa halina msingi au uhalali wowote. Waziri Mkuu huyo wa Israel amekuwa akikanusha kuhusika na kesi hiyo ya rushwa iliyoanzishwa mwaka 2019, huku wafuasi wake wakisema kesi hiyo inaendeshwa kisiasa.