SiasaKorea Kusini
Mahakama ya Korea Kusini yapinga kuendelea kuzuiwa rais Yoon
25 Januari 2025Matangazo
Taarifa hiyo imetolewa na Shirika la habari la Yonhap baada ya ombi kama hilo kukataliwa jana Ijumaa. Desemba mwaka jana, Rais Suk Yeol aliondolewa madarakani na bunge baada ya kuitumbukiza nchi hiyo katika mkwamo wa kisiasa, kufuatia hatua yake ya kutangaza amri ya kijeshi.
Soma pia: Yoon Suk Yeol agoma tena kuhojiwa na timu ya wachunguzi
Jumanne wiki hii, rais huyo alifikishwa katika mahakama ya katiba kwa mara ya kwanza, akikabiliwa na uwezekano wa kuhojiwa na majaji watakaoamuwa ikiwa anapaswa kuondolewa kabisa madarakani. Ikiwa mahakama itapitisha uamuzi dhidi ya kiongozi huyo, atavuliwa urais na uchaguzi utalazimika kuitishwa ndani ya siku 60 zijazo.