SiasaKorea Kusini
Mahakama ya Korea Kusini kuamua kuhusu hatma ya rais Yoon
4 Aprili 2025Matangazo
Mahakama hiyo itaamua iwapo rais Yoon anapaswa kuondolewa au kurejeshwa madarakani, miezi minne baada ya kiongozi huyo wa kihafidhina kuitumbukiza nchi hiyo katika mzozo wa kisiasa kufuatia uamuzi wake wa kutangaza amri ya kijeshi.
Uamuzi huo unaosubiriwa kwa hamu, unatarajiwa kutolewa katika kesi itakayopeperushwa moja kwa moja kwenye televisheni ya taifa na utahitaji kuungwa mkono na angalau majaji sita kati ya wanane wa mahakama hiyo.
Iwapo mahakama itaamuru Yoon ang´atuliwe, Korea Kusini italazimika kufanya uchaguzi wa rais ndani ya muda miezi miwili. Na ikiwa mahakama itatupilia mbali madai ya kushtakiwa kwake, kiongozi huyo atarejea mara moja kwenye majukumu yake ya urais.