Mahakama ya Kongo yamhukumu Matata Ponyo miaka 10 jela
21 Mei 2025Kufuatia mapambano ya kisheria yaliyodumua karibu miaka minne, mahakama ya katiba ya Kongo ilimkuta Matata ana hatia kwa ubadhirifu wa fedha za umma za thamani ya dola milioni 247.
Matata, ambaye alifanya kampeni dhidi ya rais wa sasa wa Kongo Felix Tshisekedi mwaka 2023 kabla kujiondoa katika kinyang'anyiro cha urais, amekuwa mara kwa mara akikanusha madai hayo akiyaeleza kuwa yamechochewa kisiasa.
Kando na Matata, jaji aliyesikiliza kesi hiyo Dieudonne Kamuleta alimhukumu mfanyabiashara wa Afrika Kusini kifungo cha miaka mitano jela na kazi ngumu na Deogratias Mutombo, ambaye wakati huo alikuwa gavana wa benki kuu ya Kongo.
Seneta wa upinzani Kongo Matata Ponyo amshtaki spika wa Seneti
Matata na Mutombo wamepigwa marufuku wasishike nyadhifa katika ofisi za umma kwa miaka mitano baada ya kukamilisha adhabu yao ya kazi ngumu.
Mfanyabiashara wa Afrika Kusini ameamriwa arudishwe kwao baada ya kutumikia kifungo chake.