UfisadiCosta Rica
Mahakama ya Costa Rica yaomba rais aondolewe kinga
2 Julai 2025Matangazo
Mwanasheria Mkuu Carlo Diaz anamshutumu Rais Rodrigo Chaves kwa kulazimisha kampuni ya huduma za mawasiliano aliyoipa kandarasi kumpatia dola 32,000 rafiki na mshauri wake wa zamani wa picha Federico Cruz.
Adhabu ya mashtaka ya rushwa kwa maafisa wa umma ni kifungo cha hadi miaka minane jela.
Ombi hilo la mahakama ya juu ambalo halijawahi kushuhudiwa linatolewa katikati ya mvutano kati ya mahakama na Chaves, mwanauchumi na afisa wa zamani wa Benki ya Dunia.