Mahakama Israel yakataa kuahirisha kesi dhidi ya Netanyahu
27 Juni 2025Wakili wa Netanyahu alimuomba jaji katika mahakama hiyo kuahirisha kesi hiyo kwa wiki mbili, akisema kiongozi huyo anahitaji kushughulikia masuala ya usalama baada ya siku 12 za vita kati ya Israel na Iran.
Mahakama imesema ombi lililotolewa halina msingi au uhalali wa kuahirisha kusikilizwa kesi hiyo. Siku ya Jumatano wiki hii Trump aliielezea kesi dhidi ya Netanyahu kuwa ya kisiasa na kutaka ifutiliwe mbali mara moja au msamaha utolewe kwa kiongozi huyo aliyomuita shujaa.
Netanyahu aahidi kupambana dhidi ya mashtaka ya rushwa
Netanyahu amemshukuru Trump kumuunga mkono katika vita vyake na Iran vilivyositishwa Juni 24 kwa makubaliano ya kusitisha vita, yaliyotangazwa na Donald Trump. Waziri Mkuu huyo wa Israel amekanusha kuhusika na rushwa huku wafuasi wake wakisema kesi yake inaendeshwa kisiasa.