Mahakama ya ICJ yatupilia mbali kesi ya Sudan
6 Mei 2025Matangazo
Mahakama ya juu ya Umoja wa Mataifa inayosimamia haki, ICJ imeitupilia mbali kesi iliyofunguliwa na Sudan dhidi ya Umoja wa falme za kiarabu, kuhusiana na mauaji ya halaiki yaliyofanyika wakati wa vita vya wenyewe kwa wenyewe.Soma pia: Sudan yaiambia korti ya ICJ kwamba UAE ndio "nguvu inayoendesha" mauaji ya halaiki
Sudan inadai kwamba Umoja wa Falme za Kiarabu,imekuwa ikitowa uungaji mkono kwa jeshi la wanamgambo la RSF ambalo limeendesha mauaji nchi humo.
Hata hivyo UAE imekanusha tuhuma hizo na mahakama ya ICJ imesema haina mamlaka ya kutowa uamuzi juu ya kesi hiyo na hivyo kuitupilia mbali.