Korti Ujerumani yausafishia njia mpango wa Merz wa ukopaji
18 Machi 2025Uamuzi huo unatoa fursa kwa bunge kufanya vikao vyake leo ili kuzingatia mapendekezo ya mshindi wa uchaguzi kutoka chama cha Kihafidhina Friedrich Merz, ya kulegeza sheria za katiba za mikopo na kuweka mfuko wa yuro bilioni 500 wa miundo mbinu.
Soma pia: Merz atetea mipango yake ya bajeti bungeni
Merz anataka hatua hizo zipitishwe na bunge la sasa, akihofia kwamba zitapingwa na bunge lijalo na hasa wabunge wa mrengo wa kulia na mrengo wa kushoto. Bunge jipya Ujerumani litaanza vikao vyake mnamo Machi 25.
Merz anasema kuna haja ya mabadiliko hayo kufanywa kwa haraka kutokana na mabadiliko ya haraka ya sera ya Marekani chini ya Rais Donald Trump, akitahadharisha pia kwamba Urusi yenye kupenda vurugu na Marekani isiyotabirika ni mambo yanayoweza kulipelekea bara Ulaya lisiweze kujitetea.