Magenge ya Haiti yawauwa wanajeshi 4 na raia 4
24 Aprili 2025Matangazo
Msemaji wa polisi ya Haiti Lionel Lazarre amekiambia kituo kimoja cha redio nchini humo kwamba mauaji hayo yamefanyika katika eneo la Kenscoff, ambalo wakati mmoja lilikuwa eneo salama nje kidogo ya Mji Mkuu Port-au-Prince.
Lazarre amesema idadi isiyojulikana ya raia pia wameuwawa katika eneo la Pacot katika huo mji mkuu. Katika video zilizochapishwa kwenye mitandao ya kijamii, watu waliojihami kwa bunduki wameonekana wakiikatakata miili kadhaa na kuvibeba vichwavya watu.
Baraza la mpito la rais nchini Haiti pamoja na afisi ya waziri mkuu, wamelaani mashambulizi hayo katika taarifa tofauti.
Polisi ya Haiti inashirikiana na kikosi cha Umoja wa Mataifa kinachoongozwa na polisi wa Kenya kukabiliana na magenge hayo, ila juhudi zao hazijafanikiwa.