magazetini nchini Ujerumani hii leo
27 Mei 2004Tuanze lakini na sheria ya uhamiaji. Na matokeo yake kwa vyama vya kisiasa. Kiroja katika mada hiyo ni kwamba wahariri wengi wanawaangalia walinzi wa mazingira wa chama cha kijani Die Grüne kua ndio walioondoka mikono mitupu.Gazeti la mjini Düsseldorf-HANDELSBLATT linalohisi waalinzi wa mazingira wameachwa kando,linaandika:
"Kufumba na kufumbua mambo yanaweza kubadilika".Wiki kama tatu hivi zilizopita walikua walinzi wa mazingira waliochochea mambo kifua mbele, walipozungumzia haja ya kuanzishwa majadiliano kuhusu sheria ya uhamiaji, bila ya hata kushauriana kabla ya hapo na washirika wao wa chama cha Social Democrat.Na hasa kiongozi wao Reinhard BÜTIKOFER alijinata na kutabasamu katika majukwaa ya kisiasa.Walinzi wa mazingira waliamini wangeshinda hatimae kwasababu walihisi fikra yao ni bora zaidi kuliko fikra ya kansela Gerhard Schröder na waziri wake wa mambo ya ndani Otto Schily.Wamekosea kwasababu walikua kansela na waziri wake wa mambo ya ndani waliozicheza karata hadi mwisho na kuwaacha kando walinzi wa mazingira."
Hata gazeti la STRAUBIGER TAGSBLATT linawaangalia walinzi wa mazingira-Die Grüne kama ndio walioondolewa patupu.Gazeti linaandika:
"Walinzi wa mazingira na walalame watakavyo.Wanaweza hata kuhoji bila ya fikra yao mazungumzo kati ya serikali na upande wa upinzani kuhusu sheria ya uhamiaji yasingepelekea pengine kupatikana maridhiano.Yote hayo hayasaidii kuwafanya wasiangaliwe kua wameshindwa.Kile walichoahidiana kansela Gerhard Schröder na viongozi wa vyama vya CDU na CSU bibi Angela Merkel na Edmund Stoiber hakina maingiliano hata kidogo na kile walichokua wakikiotea waalinzi wa mazingira.Mlango wa kuingia Ujerumani hautapanuliwa.
Gazeti la mjini Mainz RHEIN ZEITUNG linahisi sheria hiyo ya uhamiaji haistahiki jina hilo.Gazeti linaandika:
"Fursa imewaponyoka.Kile walichokubaliana kansela pamoja na viongozi wa vyama vya upinzani vya CDU na CSU hakimaanishi chochote chengine isipokua kuachana na tamaa ya serikali kuu ya muungano kuona siku moja wanabuni sheria ya uhamiaji inayoambatana na wakati.Tamaa hiyo wasocial Democrat wameachana nayo kwa masilahi ya maridhiano ambayo hayastahiki kamwe kupewa jina la sheria ya uhamiaji.Ni maridhiano yaliyokua yafikiwe kwa kila hali seuze tena waziri wa mambo ya ndani Otto Schily, baada ya kushindwa katika juhudi za kutaka kipigwe marufuku chama cha siasa kali za mrengo wa kulia NPD,amepania kujivunia ufanisi wa kudumu katika suala hilo la uhamiaji.
Mahkama ya pili ya shughuli za utawala mjini Münster imefungua njia ya kurejeshwa Uturuki kiongozi wa itikadi kali ya dini ya kiislam Metin Kaplan.Uamuzi huo unaungwa mkono na gazeti la Frankfurter Allgemeine,linalohisi Kaplan hana cha kuhofia nchini Uturuki.Gazeti linaandika:
"Ingawa hakuna anaeweza kusema kwa uhakaikifu, angalao kwa sasa kwamba mateso yametoweka moja kwa moja nchini Uturuki,lakini mageuzi ya kisiasa yanayoendelezwa na serikali ya ERDOGAN yamelengwa kupunguza hofu hizo.Serikali ya mjini Ankara haitosubutu kutumia kiini macho katika kesi dhidi ya Kaplan na waafuasi wake.Kutokana na hamu ya Uturuki ya kujiunga na umoja wa ulaya ,Ankara italazimika kumtendeya ya haki Kaplan badala ya kumtesa."
Hata gazeti la mjini Bielefeld la NEUE WESTFÄLISCHE halina pingamizi Kaplan akirejeshwa Uturuki,gazeti hilo linaandika:
"Hata mgeni asiyetakiwa kama Kaplan ambae nadharia zake zinapingana moja kwa amoja na maadili ya kidemokrasi,anaastahiki kua na kesi ya haki,kusikilizwa na maamuzi ya korti ya shughuli za utawala kufanyiwa utafiti.Lakini tukitaka kuzingatia kanuni na sheria katika nchi inaxoheshimu sheria,basi hatutakosa kuungama, vitendo vinabidi vifuate ,baada ya vuta na kivute ya kisheria iliyopindukia miaka miwili.
Hatimae tuangalie kilichosemwa na magazeti kuhusu ripoti ya mwaka ya shirika linalopigania haki za binaadam- Amnesty International.Nchi nyingi zimekosolewa ndani ya ripoti hiyo.Gazeti la Stuttgarter Zeitung linakosoa maovu yanayosababishwa na mapambano dhidi ya ugaidi.Gazeti linaandika:
"Kutumiwa kiholela silaha na jeshi la Israel kumechasfua hadhi ya nchi za magharibi sawa na visa vya wanajeshi wa Marekani na hata wa Uengereza nchini Iraq.Haijakosea Amnesty International inaposema serikali nyingi zinazooendesha mapaambano dhidi ya ugaidi zimepotelewa na maadili yao na hasa zile serikali ambazo kimsingi zilibidi kuiboresha hali ya mambo ulimwenguni.Hali hii inatisha kweli kweli.