Magaidi watiwa nguvuni Pakistan:
28 Desemba 2003Matangazo
ISLAMABAD: Katika taftishi zake za kuwasaka watu wanaoshutumiwa kuhusika na jaribio la kumwuwa Rais wa Pakistan Pervez Musharraf, polisi wamewatia nguvuni washutumiwa wanne wa itikadi kali wa Kiislamu. Washutumiwa hao wametiwa nguvuni upande wa Pakistan mkoani Kashmir, ilisema taarifa kutoka duru za maafisa wa usalama. Hapo alkhamisi washambuliaji wawili walijaribu kuiripua gari ya Rais Musharraf kwa msaada wa mabomu yaliyowekwa katika malori mawili yaliyogonganishwa na msafara wa magari wa Rais. Watu 16 waliuawa katika shambulio hilo.