Magaidi wamekamatwa UIngereza
30 Julai 2005Matangazo
London:
Polisi wa Uingereza wanaamini kuwa wamewakamata watu wote wanne wanaoshukiwa kufanya mashambulio ya mabomu mjini London. Msemaji wa Polisi amesema kuwa watu wanne waliokamatwa wamepigwa picha na kamera za doria zilizoko kwenye stesheni ya treni iliyoko chini ya ardhi muda mfupi kabla ya mashambulio hayo Alhamisi iliyopita. Scotland Yard imewakamata watuhumiwa wawili mjini London na mwingine wa tatu amekamatwa Roma, Italia. Mtu wa nne, anayeaminiwa kuwa ni Kiongozi wao, amekamatwa mjini Birmingham Jumatano iliyopita. Polisi wa Uingereza hivi sasa wanachunguza kama kuna mtandao mkubwa wa Waislamu wenye itikadi kali. Ingawaje wamefanikiwa kuwakamata watu hao wamesema kuwa kuna uwezekano wa mashambulio mengine kufanywa mjini London.