Mafuriko yauwa zaidi ya watu 100 DRC
12 Mei 2025Matangazo
Zaidi ya watu 100 wamefariki kufuatia mafuriko katika kijiji kimoja karibu na fukwe za Ziwa Tanganyika, huko Mashariki mwa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo.
Hayo yameelezwa na msimamizi wa wilaya ya Fizi katika mkoa wa Kivu Kusini Samy Kalodji, ambaye amefahamisha kwamba mafuriko hayo yameathiri kijiji cha Kasaba ambako taarifa zinaonesha hadi Jumamosi kwamba zaidi ya watu 100 wamekufa.Soma pia:Zaidi ya watu 100 wapoteza maisha kwenye mafuriko ya usiku mashariki mwa DRC
Mafuriko hayo yanashuhudiwa kwenye eneo hilo katika wakati ambapo mashambulizi ya waasi wa M23 yameongezeka katika eneo hilo la Mashariki tangu mwanzoni mwa mwaka huu.
Maelfu ya watu waliuwawa katika kipindi cha miezi miwili ya mwanzo mwa mwaka huu, kufuatia mapigano hayo.