SiasaAsia
Mafuriko yauwa watu 34 China
29 Julai 2025Matangazo
Kwa mujibu wa mamlaka za mji huo mkuu, watu 28 walipoteza maisha kwenye wilaya ya Miyun iliyoathirika vibaya na mafuriko hayo, na wengine wawili kwenye wilaya ya Yanqing usiku wa manane leo.
Zaidi ya watu 80,000 wamehamishiwa maeneo mengine kukimbia athari za mvua hiyo.
Waziri Mkuu wa China, Li Qiang, amesema mvua kubwa na mafuriko yamesababisha madhara makubwa kwenye maeneo kadhaa ya nchi na akatowa wito wa juhudi za haraka za uokozi, kwa mujibu wa shirika la habari la Xinhua.
Mvua kubwa inatazamiwa kuendelea leo kwenye miji ya Beijing na Hebei, ambayo pia iliathirika vibaya kwenye mafuriko ya mwaka 2023.