Mafuriko yasababisha vifo vya watu 19 mjini Kinshasa
14 Juni 2025Matangazo
Mafuriko makubwa yamevikumba vitongoji kadhaa vya mji mkuu wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo, Kinshasa, na kusababisha vifo vya watu wasiopungua 19 na uharibifu mkubwa.
Mvua kubwa zilizonyesha kuanzia ijumaa hadi Jumamosi, zimesababisha mafuriko na maporomoko ya udongokatika kitongoji cha magharibi mwa Kinshasa cha Ngaliema.
Meya wa eneo hilo Fulgence Bolokome, amekieleza kituo cha redio Top Congo kwamba watu 17 walipoteza maisha.
Watu wengine wawili walikufa wakati mafuriko yalipoangusha ukuta katika kitongoji cha Lemba kusini. Kambi ya polisi na daraja pia vimeharibiwa.
Mnamo mwezi wa nne mafuriko mjini Kinshasa yalisababisha vifo vya watu 22 na kukata mawasiliano ya uwanja mkuu wa ndege.