JangaAsia
Mafuriko na maporomoko ya ardhi Kashmir yauwa watu 60
15 Agosti 2025Matangazo
Takribani watu 60 wamekufa katika eneo lililo chini ya utawala wa India laKashmirbaada ya mvua kubwa iliyosababisha mafuriko na maporomoko ya ardhi, vyombo vya habari vya ndani vimeripoti.
Maafa hayo makubwa yamekifunika kijiji cha Chasoti huko Kashmir na kuwasomba mahujaji waliokuwa wamekusanyika kwa chakula cha mchana kabla ya kupanda mlima na kwenda katika eneo maarufu la kuhiji.
Mfanyakazi mmoja wa uokozi ameliambia shirika la habari la ANI kuwa walionusurika walisema kuna karibu watu 100 hadi 150 ambao huenda wamefukiwa kwenye udongo.
Tukio hilo la Alhamisi linajiri ikiwa ni wiki moja tu baada ya mafuriko na maporomoko ya ardhi kukifukia kijiji kizima katika jimbo la Uttarakhand huko Himalaya.