MAFURIKO KUSINI MWA UJERUMANI
24 Agosti 2005Gazeti linalochapishwa mjini Lüneburg likizungumzia mafuriko yaliozuka kusini mwa Ujerumani laandika:
“Hali ya hewa si ya kutegemewa-mara hivi mara vile.Kanuni hii ya kimsingi inawasumbua watu.Tangu kufanyika mapinduzi ya kiviwanda,anga limekuwa likizidi ujoto.Idadi ya wataalamu wa kisayansi ambao hawatupi lawama la kuzidi ujoto hewani mabegani mwa wanadamu wenyewe inazidi haraka kupungua.Vichwa vya habari vya hii leo vinabainisha wazi ni hali gaini ya hewa iliotanda duniani-ni hali mbaya kabisa ya hewa.Dharuba kali za vimbunga (Tornado) hazishi kuipiga Marekani,moto unaunguza misitu nchini Ureno,mafuriko katika milima ya Alpen ya Uswisi hadi kusini mwa Ujerumani.Na misiba hii ya hali ya hewa itazidi kuongezeka na kuwa mikubwa zaidi.
Marekani ambayo ndie mharibifu mkubwa wa nishati,bado iko mbali sana kugeuza msimamo wake.Nchi nyengine zinazotumia kwa wingi mno nishati kama China ,hazizimi bado kiu chao cha nishati.Tayari hii leo, hadi binadamu bilioni 1 wanahatarishwa na mafuriko.Na bila hifadhi barabara ya mazingira ya hali ya hewa,idadi ya wahanga hao itaongezeka maradufu mnamo vizazi 2 vijavyo.”-huo ulikuwea wasia wa gazeti la LANDESZEITUNG la Lüneburg.
Likiendeleza mada hii hii, gazeti la SÜDDKURIER kutoka Lüneburg laandika:
“Hali ya hewa leo ni vigumu kutabirika sawa na uamuzi wa wapiga kura.Katika milima ya Alpen huko Uswisi na Austria lakini pia kusini mwa Ujerumani,mafuriko yamezuka kwa kadiri ambayo yamefurika pia kampeni za uchaguzi na taarifa za habari.Ukumbusho wa mafuriko ya mto Order miaka 3 nyuma unajitokeza.Matokeo ya uchaguzi ujao bila shaka hayatashawishiwa na msiba huu wa kimaumbile.Bila shaka hali ya msukosuko huipa kila mara serikali nafasi ya kujijenga kwa wapiga kura,hata hivyo mkoa wa Bavaria,si mkoa wa Sachsen:Kile kilichofanikiwa 2002 katika mto Order,ni vigumu kurejewa tena miaka 3 baadae katika shina la waziri mkuu wa Bavaria Edmund Stoiber.Hatahivyo,hii haikumzuwia Kanzela Schröder kufyatuka kuzuru maeneo yalioathiriwa na mafurtiko hayo.”
Ama gazeti la NÜRNBERGER ZEITUNG linasema: watu siku hizi wanafanya mzaha huko kaskazini mwa Ujerumani wanaposema:
“Kanzela Schröder hakukawia kuvaa mayatu yake ya mpira ili kujitumbukiza mkoani Bavaria kwenye mafuriko ili kukuza heba yake kama alivyofanya 2002 yalipozuka mafuriko m akubwa ya karne hii kandoni mwa mito Order na Elbe.Kuonesha mshikamano na waliofikwa na maafa na kuwanyoshea mkono wa misaada kuliisaidia serikali yake.
Lakini huko Eschenlohe,Kempten na siku zijazo Donau,wakaazi wa huko hawatomhitaji Kanzela huyu na mfanya kampeni ya ucvhaguzi kwa kutumia misiba ya mafuriko.”_ni wasia wa NÜRNMBERGER ZEITUNG.
Likitugeuzia mada,gazeti la Cologne: STADTANZEIGER juu ya matumaini ya kustawi tena kwa uchumi wa Ujerumani laandika:
“Hata matumaini ya kustawi tena kwa uchumi kwa robo-ya tatu ya mwaka huu yakinawiri namna gani, kwa kipindi kirefu kijacho,kufufuka kwa uchumi kutategemea mno matumizi ya watu wa kawaida.Raia watafungua mikaja yao na kutumia wakianza kuwa na hisia waweza kupanga hali zao za baadae..Kwani, uchumi wa Ujerumani ungali ukijikuta njia- panda kati ya kuselelea kuzorota na kustawi.”