Watu 30 wamefariki dunia Kinshasa kufuatia mafuriko yaliyoukumba mji huo mwishoni mwa wiki. Serikali inawalaumu waliojenga makaazi karibu na mito na imetishia kuwafurusha. Mto Ndjili ambao unapitia sehemu moja ya mji huo mkuu wa Jamhuri ya Kidemokrasi ya Kongo, ulifurika na kuvunja kingo zake. Gavana wa Kinshasa Daniel Bumba Lubaki anasema miundombinu ya maji imeathirika.